24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MANGULA AWASHANGAA VIONGOZI WA DINI

Na Elizabeth Kilindi-Njombe


MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula, amewashangaa viongozi wa dini na kusema sasa wamekuwa sehemu ya kuchochea migogoro ya kisiasa badala ya kusuluhisha.

Kauli hiyo aliitoa juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Kinenulo wilayani Wanging’ombe, mkoani Njombe, ambapo alisema kama viongozi wa dini hawatakuwa makini wanaweza kuligawa taifa.

Alisema viongozi hao wangekuwa wanatumia nafasi hizo kuwahamasisha vijana juu ya kuwainua kiuchumi kuliko kuingilia masuala yanayoweza kusababisha machafuko.

“Mambo ya siasa waachie wanasiasa maana wamechukua majukumu ya uchonganishi badala ya usuluhishi, wana waumini aina mbalimbali wakiwemo vijana hivyo ni bora wawaelimishe njia ya kuwainua kiuchumi,” alisema Mangula

Alisema baadhi ya wanasiasa wanawatumia viongozi wa dini kuleta machafuko nchini, hali ambayo ni tofauti na kiapo cha viongozi hao.

“Baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiwatumia viongozi wa dini ili kutuletea machafuko, hata hao viongozi wa dini tunachojua nao wana kiapo chao ambacho kinawakataza kujihusisha na masuala ya siasa,” alisema.

Akizungumzia utendaji kazi wa Rais Dk. John Magufuli, alisema kiongozi huyo anatekeleza ilani ya CCM pamoja na mambo yote waliyokubaliana ndani ya chama.

“Rais lazima awe mkali kwa sababu ilani inaelekeza hivyo huwezi kumkamata fisadi huku anawaimbia nyimbo na kumpigia kinanda. Nguvu lazima itumike kuhakikisha mambo tuliyoyapanga kwenye ilani yanatimia,” alisema  Mangula.

Alisema CCM haina mgogoro na chama chochote cha siasa,  badala yake vyama hivyo vipo kwenye mpango wa kukwamisha utekelezaji wa ilani ya chama hicho tawala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles