26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mangula ataka vijana wajiajiri

FRANCIS GODWIN, IRINGA 

MAKAMU   mwenyekiti wa  Chama  cha Mapinduzi (CCM ) Tanzania Bara, Philip Mangula amewataka vijana kufuta fikra za kufikiria kuajiriwa badala yake wafikirie kujiajiri wenyewe.

Mangula  alitoa kauli  hiyo juzi, wakati wa ufunguzi wa chuo cha UVCCM Ihemi Iringa, akisema kuwa vijana nchini wanapaswa kubadili mitizamo ya kusoma ni kuajiriwa bali wasome wakijua watajitegemea na chuoni hapo watafundishwa namna ya kujiajiri kwani ajira kubwa ni kilimo.

 “Mnapokuja kwenye mafunzo hapa chuoni nataka mfute kabisa mawazo ya tunajifunza ili tukaajiriwe, hapa ni sehemu ya mafunzo ya kubadilisha fikra na mitizamo ya kwamba, kusoma ni kuajiriwa,” alisema Mangula.

Akizumgumza katika uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally, alitangaza bodi ya muda ya ushauri wa chuo hicho itakayofanya kazi kuanzia sasa, ambapo wajumbe hao watakuwa katika bodi hiyo kwa nafasi zao.

Kwa upande wake, Mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa, waziri  mkuu mstaafu Mizengo Pinda alisema moja ya malengo ya chuo hicho ni kujenga hisia ndani ya vijana juu ya siasa ya nchi hii kwa maslahi ya Watanzania.

Alisema ni muhimu vijana kutambua uzalendo ni kitu gani hivyo yanapoanza mafunzo ni muhimu kujikita zaidi katika siasa na itikadi ili waweze kujua Taifa linataka nini na wao wajibu wao ni nini.

Eneo hilo la uwekezaji wa miradi 21 ya vijana tayari limeanza kazi na katika uzinduzi wa eneo hilo, Mangula pia alizindua Kiwanda Cha ufundi stadi kushona kilicho chini ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na kukagua kilimo cha nyanya na mbogamboga chuoni hapo, huku katibu mkuu akiweka jiwe la msingi wa ujenzi wa ukumbi chuoni hapo.

Hafla  hiyo, ilihudhuriwa na  viongozi na wanachama wakiongozwa na mjumbe wa Kamati Kuu Maalim Juma Kombo, Mwenyekiti wa UVCCM  na Mjumbe wa Kamati Kuu Kheri James, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM  Tabia Mwita, Katibu Mkuu wa UWT Queen Mlozi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi  Erasto Sima

Wengine  ni wajumbe  wa Halmashauri Kuu Taifa wakiongozwa na Salim Abria Asas  mwenyeji, mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa  Arif Abri, viongozi wa mila, viongozi wa dini, wakuu wa mikoa ya Iringa Ally Hapi  na Mkuu Mkoa wa Njombe Christopher  Ole Sendeka  pia  waziri  wa  ardhi  nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi  na  wengine   pamoja na wakuu wa wilaya za mkoa wa Iringa na wabunge .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles