27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mancini awatisha wapinzani Euro 2020

PALERMO, ITALIA

BAADA ya timu ya taifa ya Italia kufanikiwa kufuzu michuano ya Kombe la Euro 2020, kocha wa timu hiyo Roberto Mancini, amedai ubora w akikosi chake utawafanya wapinzani wasiingize timu uwanjani.

Timu hiyo ilikuwa kundi J, hivyo juzi ilifanikiwa kufuzu baada ya kuwachapa wapinzani wao Armenia mabao 9-1, huko jijini Palermo nchini Italia.

Katika mchezo huo Italia walionekana kuwa kwenye kiwango cha hali ya juu na kuwafanya mashabiki waamini kuwa timu hiyo ina nafasi kubwa ya kwenda kutwaa ubingwa kwenye michuano hiyo.

Kichapo hicho walichokitoa Italia, kimemfanya kocha wa timu hiyo Mancini aamini hiyo ni salamu kwa wapinzani ambao watakuwa kundi moja na ikiwezeka wasipeleke timu uwanjani.

“Sijui kama wapinzani wana wasiwasi au hawana, nadhani kuna timu bora ambazo tutakwenda kukutana, Ufaransa ni miongoni mwa timu bora iliwahi kufika fainali kwenye Euro, mwaka jana ilitwaa ubingwa wa Kombe la Dunia, ina wachezaji wengi chipukizi, hivyo ni timu bora kama ilivyo Hispania.

“Ubelgiji ipo vizuri imekuwa ikiongoza kwa ubora, England na wao wapo vizuri, lakini Italia ina historia yake, sidhani kama kuna timu ambayo itakuwa tayari kukutana na Italia kwa urahisi, labda watakuwa hawatuogopi, lakini ninaamini kama timu zitaambiwa watafute wa kucheza nao Italia watatukimbia,” alisema kocha huyo.

Kocha huyo aliongeza kwa kuwapongeza wachezaji wake kwa kiwango walichokionesha kwenye mchezo huo huku akiamini wataendelea kuwa bora siku hadi siku.

“Kuna wachezaji wengi kwenye kikosi changu ambao ni wachanga, lakini wamekuwa wakibadilika siku hadi siku, kucheza kwenye michezo mikubwa ya kimataifa kunawafanya wabadilike, kilichobaki kwa sasa ni muda tu.

“Tutaona nini kitatokea mwakani kwenye michuano hiyo ya Euro, hatukuweza kushinda michezo yote 10 ya kuwania kufuzu, lakini kwenye michuano yenyewe tutauwasha moto wetu,” aliongeza kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles