29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Manchester City yaangukia pua England

guardiolaLONDON, ENGLAND

TIMU ya Manchester City jana kwa mara ya kwanza ilipoteza pointi tatu katika mchezo wa Ligi Kuu England, baada ya kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Tottenham katika Uwanja wa  White Hart Lane.

Kabla ya mchezo huo, kikosi hicho cha kocha  Pep Guardiola kilikuwa na uwiano  mzuri baada ya kushinda michezo yote sita ya ligi kuu na kuongoza ligi hiyo.

Manchester City ilicheza dhidi ya wapinzani wao bila ya kuwa na  nyota wake,  Kevin De Bruyne, wakati wapinzani wao wakiwatumia  Eric Dier, Mousa Dembele na Danny Rose.

Kipigo hicho kimefuatia baada ya kutoka sare 3-3  mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya  timu ya Celtic.

Mabao mawili ya Tottenham yalipatikana kipindi cha kwanza bila ya nyota wao, Harry Kane na Vincent Janssen, waliokuwa benchi.

Safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ilikuwa ikiongozwa na Heung-Min Son ambaye alifanikiwa kushinda mabao mawili, huku bao la tatu likifungwa na

Dele Alli kipindi cha pili na kuwachanganya zaidi Manchester City.

Licha ya Guardiola kufanya mabadiliko kipindi cha pili na kuwaingiza Ilkay Gundogan na  Kelechi Iheanacho, timu hiyo haikufanikiwa kupata bao hadi mpira unamalizika dakika 90.

Wakati Manchester City wakiambulia kipigo hicho, majirani zao Manchester United walipata sare ya bao 1-1 dhidi ya Stoke  City.

Katika mchezo huo, Rooney  aliingia kipindi cha pili dakika ya 67, akichukua  nafasi ya Juan Mata, huku Anthony Martial akiwa mbadala wa Jesse Lingard.

Bao la Manchester United lilifungwa na Anthony Martial dakika ya 69, likiwa bao la kwanza kwa mchezaji huyo tangu msimu uanze, huku Joe Allen akisawazisha bao hilo dakika ya 81.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles