24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Manchester City mikononi mwa Ronaldo

RonaldoLONDON, ENGLAND

TIMU ya Manchester City inatarajia kucheza dhidi ya timu ya Real Madrid katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA).

Ikiwa katika mbio za kucheza fainali ya UEFA itakayochezwa Mei 28 mwaka huu katika Jiji la Milan, nchini Italia, Manchester City ilifanikiwa kuiondosha timu ya Paris Saint Germain (PSG) katika robo fainali kupitia mchezaji wake wa nafasi ya kiungo, Kevin De Bruyne, ambaye alifunga bao 1-0 ikiwa nyumbani na kufanya jumla ya mabao katika michezo yote kuwa 3-2.

Timu hiyo itaanza kuchanga karata yake katika uwanja wa nyumbani Aprili 26/27 kabla ya kuelekea ugenini katika Uwanja wa Bernabeu baada ya wiki moja.

Itakutana na Madrid ambayo ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano ikiwa nyumbani baada ya kufungwa ugenini jumla ya mabao 2-0 dhidi ya timu ya Wolfsburg ya Ujerumani.

Wachezaji wa timu hiyo, Ronaldo na Gareth Bale ambao waliwahi kucheza katika Ligi Kuu England, watarejea England wakiwa katika mitazamo tofauti.

Mchezo mwingine wa nusu fainali utakuwa kati ya Atletico Madrid ambayo ilimtoa bingwa mtetezi Barcelona, dhidi ya Bayern Munich iliyoko chini ya Pep Guardiola ambaye itakuwa nusu fainali yake ya mwisho kabla hajatimkia timu ya Manchester City msimu ujao.

Hata hivyo, kuna historia kati ya Bayern Munich na Atletico Madrid wakati ilipokutana mwaka 1974 katika fainali ya Kombe la Europa.

Mchezo wao wa kwanza katika Uwanja wa Heysel uliopo mji wa Brussels nchini Ubelgiji zilitoka sare ya 1-1 baada ya muda wa ziada kabla ya Bayern haijashinda  katika mchezo wa marudiano mabao 4-0 yaliyofungwa na mshambuliaji wa timu hiyo, Gerd Muller na Uli Hoeness.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles