24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Man United yampandishia dau Pogba

MANCHESTER, ENGLAND

MANCHESTER UNITED wameongeza dau la Euro milioni 30 katika thamani ya kiungo wao, Paul Pogba( 26), na sasa wanataka dau la Euro milioni 180, ili kumruhusu kujiunga na timu inayomtaka.

Mfaransa huyo, ameonyeha nia kutaka kuondoka ndani ya timu hiyo katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi, huku klabu za Real Madrid na Juventus zikikaa mkao wa kula kumchukua.

United tayari imeshaweka wazi kuwa, haina mpango wa kumuuza mchezaji huyo waliomnunua kutoka Juventus kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 89 miaka mitatu iliyopita.

Hivyo, kuongeza dau hilo ni moja ya mikakati ya kuzikatisha tamaa klabu zinazowinda saini ya kiungo huyo aliyeisadia Ufaransa kutwaa Kombe la Dunia mwaka jana nchini Russia.

Ripoti kutoka gazeti la Mail la Uingereza, zinaeleza kuwa, Juventus imejitoa katika mbio za kumwania Pogba na kuacha fursa hiyo kwa Madrid kumsaini.

Ilifikiriwa kuwa, United ingehitaji dau la Euro milioni 150, kwa ajili ya kumuamchia Pogba, ambaye anaungwa mkono na wakala wake, Mino Raiola katika mpango huo wa kutimka Old Trafford.

Raiola anataka kumuhamisha mteja wake huyo, ili kujipatia kiasi kikubwa cha fedha kama alivyofanya wakati alipohamia United, akitokea Juventus.

Wakala huyo maarufu alinunua kipengele cha mkataba wa Pogba kilichomruhusu kuondoka kwa Vibibi Kizee hao wa Turin na kuvuna pauni milioni 20 kwa kufanikisha uhamisho huo.

Hivi karibuni, Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Ole Gunnar Solskjaer, akiwa nchini Australia kwenye maandilizi ya msimu mpya, alisema mchezaji huyo hauzwi.

Alisema; “ Man United ni timu kubwa hivyo hatuwezi kumuuza Pogba wala mchezaji wetu mwingine yeyote muhimu kikosini.

“Kwa vile ninajua kuwa hakuwa na ofa iliyoletwa kwa mchezaji yeyote, sisi ni Man United na hatumuuzi Pogba, wala hakuna biashara kama hiyo.

“Paul hajawahi kuwa na wasiwasi na mimi, anafanya kazi kwa bidii, ni mchezaji mwenye weledi na kijana wa kujivunia, jibu ni lile lile tena, siwezi kukaa hapa kuzungumza juu ya kile Paul na wakala wake wanasema, bado miaka michache imebaki kwenye mkataba wake na yupo katika kiwango bora.

“Niko hapa kuzungumza kuhusu maandalizi ya msimu mpya ujao, Paul hakuwa nje ya timu, mara zote nimekuwa nikimpa baraka zote na hakuwahi kuniambia chochote, wakala huzungumza wakati wote na hatujawahi kupokea ofa yeyote, hicho ndicho nachoweza kuzungumza kuhusu jambo hili.

“Sijaongea na Raiola, kuna mawakala ambao kila mmoja anamuangalia mchezaji wake, tuna wachezaji na timu iwaangalie.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles