23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Man United wamtaka Pogba kuondoka

MANCHESTER, England

MASHABIKI wa Manchester United wameutaka uongozi wa klabu hiyo kuachana na kiungo wao, Paul Pogba, mara baada ya kumalizika kwa msimu huu, kutokana na mchezaji huyo kuonesha mapenzi na klabu ya Real Madrid.

Mapema wiki hii, mchezaji huyo alishindwa kuzuia hisia zake na kuweka wazi kuwa, ndoto zake siku moja ni kuja kuwa mchezaji wa Real Madrid, huku akidai kila mchezaji ana ndoto za kuitumikia timu hiyo kutokana na ukubwa wake.

Mashabiki hao wanaamini mchezaji huyo ana lengo la kutaka kuungana na kocha Zinedine Zidane, ambapo wote wanatoka nchi moja, Ufaransa.

“Kama ninavyosemwa kila siku, Real Madrid ni sehemu ya ndoto kwa kila mchezaji. Ni moja kati ya klabu kubwa duniani, hasa kwa sasa Zidane ndiye kocha wao, hivyo kila mchezaji anatamani kuja kuitumikia timu hiyo kwa wale ambao wanapenda soka.

“Lakini kwa sasa mimi ni mchezaji wa Manchester United, hatujui nini kinaweza kutokea hapo baadaye, nipo Manchester United na nina furaha kuwa hapa,” alisema Pogba.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alikuwa anahusishwa kuwindwa na klabu zote, Real Madrid na Barcelona. Hivyo kutokana na kauli hiyo, inaonekana kumuweka katika wakati mgumu hasa kwa mashabiki wa timu hiyo, ambao wanadai ni vizuri akaondoka kwa kuwa tayari ameonesha mapenzi ya wazi na Madrid.

Pogba alianza kutangaza nia ya kutaka kuondoka Manchester United tangu alipopishana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho na kumfanya mchezaji huyo akose namba kwenye kikosi cha kwanza, lakini baada ya kuondoka kocha huyo na nafasi yake kuchukuliwa na Ole Gunnar Solskjaer, Pogba amekuwa akipata nafasi ya kudumu, lakini bado mashabiki wanautaka uongozi kuachana na mchezaji huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,411FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles