29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

Man United wamalizana na Mourinho

MANCHESTER, ENGLAND

UONGOZI wa klabu ya Manchester United, umemalizana na aliyekuwa kocha wao, Jose Mourinho, kwa kumlipa kiasi cha pauni milioni 15, ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 44 za Kitanzania.

Kiasi hicho cha fedha wamemlipa ikiwa ni sehemu ya kuvunja mkataba wake Desemba 18, mwaka jana kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55, alifukuzwa kazi baada ya kuwa ndani ya klabu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu.

Kulikuwa na taarifa kwamba, baada ya Mourinho kuvunjiwa mkataba, alikuwa hawezi kujiunga na klabu nyingine yoyote hadi wamalizane na United kwenye suala la malipo.

Lakini chanzo cha habari cha karibu kutoka kwa Mourinho kilisema kwamba, hakuna tatizo lolote kati ya kocha huyo na Manchester United, ana uhuru wa kujiunga na timu yoyote, ila hana haraka ya kufanya hivyo.

“Mourinho amedai hana haraka ya kujiunga na klabu yoyote baada ya kumalizana na Manchester United, kwa sasa anataka kupumzika kwanza, lakini kuna uwezekano mkubwa wa kurudi viwanjani mara baada ya kumalizika kwa msimu huu,” kilisema chanzo hicho.

Kabla ya Mourinho kuondoka Manchester United, mkataba wake ulikuwa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu wa 2019-20.

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid ambao waliwahi kufanya kazi na kocha huyo kuanzia mwaka 2010-2013, kwa sasa wanahusishwa tena kutaka kumrudisha kocha huyo kwenye viwanja vya Santiago Bernabeu.

Msimu huu Real Madrid wamekuwa katika kipindi kigumu kutokana na matokeo wanayoyapata tangu kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Zinedine Zidane, pamoja na mshambuliaji wao hatari, Cristiano Ronaldo, ambaye amejiunga na Juventus.

Katika msimamo wa ligi, Real Madrid ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, wanashika nafasi ya tano wakiwa na pointi 30 baada ya kucheza michezo 18, huku wapinzani wao Barcelona wakiongoza wakiwa na pointi 40.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles