26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mamlaka ya Maji Safi Tanga kuanza kutumia mita zinazojisoma zenyewe

NA OSCAR ASSENGA-TANGA

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Tanga (Tanga Uwasa), imesema inafikiria kuanza kutumia mita za kisasa ambazo zinasoma ankara za maji zenyewe na kutuma taarifa kwenye kanzi data ofisini.

Hayo yalisemwa juzi na Ofisa Ankara wa Tanga Uwasa, Daudi Mkumbo, wakati akizungumza kwenye mkutano na wananchi wa Kata ya Duga jijini Tanga kutoa elimu kuhusu huduma zao.

Mkumbo alisema mita hizo zitakuwa zimefungwa chombo ambacho kitakuwa na uwezo wa kujisoma zenyewe hali ambayo itarahisisha usomaji.

 Alisema anaamini uwepo wa mita hizo utaondoa changamoto kwa baadhi ya wateja ambao wanadai wasomaji hawafiki maeneo yao.

 “Kwa sasa kuna teknolojia ambayo mtu hataweza kusoma mita ya maji kwa umbali wa mita zaidi ya 600,  ina maana ndani ya 600 ndio mtu anaweza kusoma. Maana yake kila mita ya maji itakuwa imefungwa kifaa hicho cha GPS ya eneo na ile mita ilipo atakuwa anatambulika na msomaji akifika ndani ya mita 600 hawezi kudanganya,” alisema.

Alishauri wananchi wa maeneo hayo kuacha tabia ya kutokuacha mabomba wazi wakati wanasubiri maji kwani hiyo ndiyo inaweza kuwa chanzo kikubwa cha kupata bili kubwa ambayo haihusiani na matumizi ya maji.

 “Kipindi ambacho maji yamekatika bomba linajaa upepo, hivyo wakati maji yanaporudi yakiwa na msukumo ule upepo ndio ambao unatangulia kabla ya maji unaozungusha mita na hiyo ndio chanzo cha bili kuwa kubwa. Ukifungulia maji wakati hamna maji utasababisha bili kuwa kubwa wakati maji yanaporudi huo ni ushauri,” alisema.

Mmoja wa wananchi wa eneo hilo, Selemani Rashid alishauri; “muweke utaratibu kwamba wasomaji wanapokwenda kusoma mita, wakutane na wahusika ili washuhudie namna zinavyosomwa ili kuonda dhana kwamba hawapiti.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles