23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mamlaka ya dawa yateketeza bidhaa bandia 3,000

Aveline Kitomary – Arusha

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Kaskazini, imeteketeza bidhaa bandia 3,160 za dawa, vifaa tiba na vitendanishi vilivyokaguliwa katika vituo vya forodha.

Hayo yalisemwa jana jijini hapa na Meneja wa TMDA Kanda ya Kaskazini, Proches Patrick.

Alisema bidhaa hizo ambazo hazikuweza kukidhi vigezo vinavyotakiwa, zimeteketezwa katika kipindi cha miaka minne.

Hata hivyo Patrick alisema kiwango cha utoaji kibali kimeongezeka ambapo jumla ya vibali 1,160 vimetolewa kwa kipindi cha miaka minne.

Akizungumza wakati wa kampeni ya ‘Tunaboresha Sekta ya Afya’ inayoendeshwa na maofisa mawasiliano wa taasisi zilizoko chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Patrick alisema matumizi ya teknolojia pia yamerahisisha majibu ya vibali kutolewa ndani ya saa 24.

“Tunatoa elimu ya udhibiti kwa njia mbalimbali, kwanza tunatumia vyombo vya habari na pia elimu ya kuonana ana kwa ana, lengo ni kwamba ukiwa unatumia bidhaa ujue matumizi na ubora wake ukoje, hii ni kwa wafanyabiashara na wananchi.

“Ili uweze kuingiza mzigo lazima uwe na kibali, sisi tunatoa kwa kutumia mfumo wa kielektroniki katika mtandao wa TMDA, unaomba kibali halafu unatuma halafu tunapokea kibali, hii imepunguza muda,tulikuwa tunatumia siku tatu ila sasa tunatoa ndani ya saa 24.

“Tulichukua sampuli 243 za dawa na kupima ubora, usalama na ufanisi wake kwenye maabara, hapa jumla ya maeneo 5,017 yalikaguliwa katika halmashauri 21 tunazosimamia na tumesajili maeneo 514 ya biashara,” alisema Patrick.

Patrick alisema kuwa TMDA inaendelea kuwahamasisha wadau mbalimbali ili wawekeze katika ujenzi wa viwanda vya dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles