23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mamlaka dawa za kulevya yatoa kemikali kutengeneza vitakasa mikono

Na BRIGHITER MASAKI-DAR ES SALAAM

MAMLAKA  ya  Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, wamemkabidhi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Lita Laki Moja na sabuni za kemikali kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono (sanitizer). 

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika  Bohari ya Dawa ya MSD jijini Dar es Salaam, wakati akipokea kemikali hizo, Makonda alisema alipambana na dawa za kulevya na mtiti wake ulionekana. 

“Napenda kuwapongeza Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa ya kulevya kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa kupambana na kuweza kuzitunza kemikali hizi kwa kipindi chote hadi kufika kwa Mkemia Mkuu.

“Kwa nafasi yangu nilishawahi kuingia kwenye vita ya kupambana na madawa ya kulevya na changamoto zake nazijuwa, juzi wamekamata tena dawa na tunaona hali ya mtaani inazidi kuwa nzuri, katika mazingira yetu yote”

“Hilo mnalolifanya katika mazingira yote haya malipo yapo kwa Mungu na tunashukuru kwa vipimo vilivyoonyesha kuwa tunaweza kutengeneze ‘sanitaizer’ na kufanya ipatikane kwa watu wote na wa hali zote”

“Mkemia amesema dawa hizo zitakazotengenezwa zitasaidia kupunguza tatizo la ‘sanitaizer’ kwa asilimia 40 na itasaidia kupatikana  hadi kwa watu wa hali ya chini.

“Hadi mpika vitumbua, bodaboda na mama lishe watakuwa na uwezo wa kupata na kuweza kujikinga na ugonjwa wa Corona na kuondokana na dhana ya kusema sanitaizer ni kwa ajili ya matajiri peke yake”alisema Makonda

Aidha alisema kuwa viwanda vitakavyopewa kemikali hizo za kutengenezea vitakasa mikono ni vile vilivyosajiliwa na Serikali tu.

“Viwanda ambavyo kwa kiasi kikubwa kinauza bidhaa zake kwa wingi na tutasimamia bidhaa hizo kuuzwa kwa bei itakayosaidia watu wote wapate kwa kuwa lengo ni kupambana na Corona.

” Kwa upande wake, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Fidelis Mafuniko, alisema kiwango kilichopo katika kemikali hiyo kinafaa katika utengenezaji wa vitakasa mikono.

Alisema kemikali hizo watazigawa katika viwanda ambavyo vinatengeneza vitakasa mikono ili iwasaidie wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles