25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mamilioni kiganjani mwako na Bingo ya Parimatch

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya michezo ya kubahatisha Parimatch imeamua kuwapa fursa mpya wateja wake kwa kucheza Casino kiganjani ambayo imesheheni zaidi ya michezo 200 mikali ndani yake ikiwemo BINGO na KENO ambazo zimeshika kasi kwa kupendwa na watu wengi.

Hayo yamebainishwa na Afisa Habari na Mawasiliano kwa Umma wa Parimatch, Ismael Mohamed wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano mfupi na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 12, 2022 na kusema kwamba kupitia tovuti yao ya Parimatch wataweza kufurahia kucheza na kushinda michezo mingi ya Bingo kwa dau dogo la kuanzia Sh 400.

“Hakuna haja tena ya kuendelea kusubiria hadi wikiendi ndio utengeneze pesa kwa kubeti kwenye soka, sisi kama Parimatch tumeamua kuwaletea Casino yenye michezo zaidi ya 200 tofauti tofauti yenye kukupa msisimko ambao hujawahi kuupata huko nyuma. Kwa mfano unaweza kucheza mchezo wa Don Bingote ambayo inaanzia dau la Shilingi 400 na kila sekunde watu wanavuna mkwanja wa maana yaani huu sio utani watu wanapiga kiukweli,” amesema Mohamed.

Aidha, Mohamed aliendelea kwa kusema kwamba “utofauti wa Casino ya Parimatch unaanzia kwenye ubora wa mfumo wetu ambao unaendeshwa kisasa zaidi na kuwezesha kupata malipo kwa haraka zaidi sekunde chache tu mara tu unaposhinda na hakuna masuala ya kusubiria hadi kukuche asubuhi,”.

Aidh,a Mohamed pia aliwasisitizia wadau wa Parimatch kuendelea kufurahia kucheza Virtual game na michezo mingine mbalimbali kupitia tovuti yao ambayo itaweza kuwaburudisha na kusisimua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles