24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 25, 2022

Mamia waandamana wakisubiri hotuba ya Duterte

 MANIPA, PHILIPPINES

MAMIA ya Wafilipino wameandamana katika Mji Mkuu wa Manila, wakipinga sheria mpya ya kupambana na ugaidi na masuala mengine. 

Maandamano haya yamefanyika licha ya kitisho cha polisi cha kuwakamata waandamanaji kuelekea hotuba ya kila mwaka kwa Taifa ya Rais Rodrigo Duterte. 

Katika mji wa Quezon Kamanda wa Polisi, Debold Sinas alisema waandamanaji wanne waliokuwa kwenye gari la abiria walikamatwa ila mamia walikusanyika katika chuo Kikuu cha Ufilipino. 

Makundi mengine ya waandamanaji waliandamana kwa kuchapisha video mitandaoni ikiwemo video moja inayotishia kuichoma sanamu ya Rais Duterte.

Uongozi ulipiga marufuku mikusanyiko ya zaidi ya watu kumi ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona. 

Waandamanaji lakini walisema Serikali inatumia janga hilo ili kuzuia ukosoaji mkubwa katika masuala kadhaa ikiwemo jinsi ilivyolishughulikia janga hilo la virusi vya corona.

AP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,139FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles