24.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 29, 2023

Contact us: [email protected]

Mambosasa: Gwajima si mtuhumiwa, tumeanza uchunguzi

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeanza uchunguzi wa picha na video ya ngono inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidhaniwa kuwa ni ya Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Mei 8, na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa imesema Mei 7 mwaka huu zilisambazwa picha na video na watu wasiofahamika zikidhaniwa ni za Askofu Gwajima na mwanamke asiyefahamika.

“Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa picha na video hizo mara moja na linapenda kuwataarifu wananchi kuwa Gwajima sio mtuhumiwa bali ni muathirika wa tukio hilo kwani jambo hili linaweza kufanywa na mtu yeyote kwa nia ya kumuharibia mtu heshima yake kwa jamii na waumini wake.

“Aidha Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuacha kusambaza video hiyo kwani ni kosa la jinai na linawataka waumini wake kuwa watulivu kwani uchunguzi unaendeleaje ili kubaini aliyesambaza video hiyo na lengo la kufanya hivyo,” imesema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles