25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MAMBO YATAKAYOKUFANYA USOME KWA RAHA

Na FARAJA MASINDE


 

chuoHUENDA kwa namna moja ama nyingine ulikosa fursa ya kusoma nje ya nchi mwaka huu, huna ulichopoteza kwani mwaka 2017 huu hapa.

Inawezekana ulikuwa umepata chuo au la au umepanga kuanza mwakani basi makala haya itakuwa na msaada mkubwa kwako.

Kabla hujatuma maombi ya kuomba kujiunga na vyuo vikuu vya ng’ambo hatua hizi tano zitakuwa ni nguzo kubwa kwako kwani zitakujengea mazingira ya kujiamini wakati wote kabla na baada ya kujiunga na chuo.

Kwani kuna baadhi ya wanafunzi ambao huingiwa na hofu wanapokuwa kwenye vyuo vya nje ya nchi kulingana tu kwamba hajui mazingira vizuri.

Kwa kawaida dirisha la vyuo vingi vya nje kwa mwaka wa masomo hufungwa Januari 15 nyakati nyingine hivyo bado unanafasi, pia pitia kwenye tovuti mbalimbali kupata ujuzi wa kile unachotaka kwenda kukisoma ili iwe rahisi kwako.

 

Hakikisha unakifahamu chuo vizuri

Ndiyo hii ni hatua ya kwanza na muhimu kwa mwanafunzi kabla ya kutuma maombi ya kuomba chuo kwani wapo baadhi ambao wamekuwa wakiomba nafasi za kusoma nje kwenye vyuo mbalimbali kwa kubahatisha bila kufahamu vyema chuo anachotaka kwenda kusoma.

Kwa mwanafunzi husika kufanya tafiti na kujua mazingira ya chuo anachotaka kwenda kusoma itamsaidia kufanya chaguo lililosahihi,  hivyo  ni vyema ukatumia muda wako kuangalia mazingira yote ya chuo unachohisi kinakufaa ikiwamo pia kuangalia matawi yake yote(Campas) na hata miji kilichopo mambo ambayo unaweza kuyapata kupitia tovuti za chuo husika.

Ni jambo la msingi na muhimu kujua mazingira ambayo unatarajia kuwapo kwa kipindi cha miaka kadhaa ya taaluma yako, lakini pia hii itakusaidia iwapo utakuwa na swali la ziada juu ya kile ulichokiona kwenye tovuti hiyo kuhusiana na chuo hicho kuweza kuuliza na kupatiwa ufumbuzi kwa haraka kabla hujatuma maombi au kujiunga.

 

Soma yanayohusiana na taaluma yako

Licha ya kwamba huenda labda tayari unaitambua kozi unayotaka kwenda kusoma lakini lazima ujue kuwa kuna topiki nyingine mbalimbali ndani ya hicho unachopanga kwenda kukisoma ambapo huenda baadaye ukakuta ni mambo mageni kwako licha ya kwamba unakitambua vyema unachokisoma.

Hivyo, ili kuepukana na ugeni wa vipengele mbalimbali ndani ya taaluma yako hiyo ni jambo la busara iwapo utahakikisha kuwa unatumia muda wako kupitia kwenye mitandao mbalimbali kujua kozi unayotaka kwenda kusoma kwa kina zaidi.

Ni lazima utambue kuwa mara nyingi maudhui ya yale yanayofundishwa yamekuwa yakitofautiana hasa kwenye vyuo hivi vya ng’ambo kutoka kimoja kwenda kingine, hii pia hugusa aina ya ufundishaji, Kingereza wanachotumia kinaweza kuwa tofauti na kile unachokitambua wewe.

Hivyo, hakikisha kuwa unajiridhisha iwapo aina ya mtaala wa chuo husika utaendana na wewe sawasawa kabla ya kujiunga na chuo.

Tambua kuwa iwapo utazingatia hatua hizo zote ikiwamo kusoma mazingira vyema na aina ya masomo yaliyopo kwenye kozi unayotaka kwenda kusoma, ni wazi kuwa huwezi kukumbana na ugeni wowote kwenye siku yako ya kwanza chuoni na darasani kwa ujumla.

 

Ongea na wanafunzi wengine

Unajua kuwa mnaweza kujikuta mpo watu wengi kwenye boti moja kama wewe ila hamfahamiani, hii inamaana kwamba unaweza kujikuta kumbe kuna watu wengi ambao nao wametuma au wanafikiria kutuma maombi kwenye chuo unachotaka kuomba wewe tena kwa kozi ile ile.

Unaweza kuwapata kupitia Tovuti ya chuo ambapo huko unaweza kujikuta unaelekezwa watu ambao wako karibu na wewe ambao wamehitimu masomo kama yakwako au wengi wapo chuo hivyo unakuwa umepata pa kuanzia kuliko kusema ukae kimya wewe na kozi yako kwani unaweza kujikuta unafanya mambo rahisi kuwa magumu zaidi.

Pitia pia kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook  kuangalia kama kuna grupu la watu waliosoma kozi hiyo ya kwako hapo chuoni.

 

Fanya maandalizi ya mwisho

Hii ni hatua muhimu mno katika kuhakikisha kuwa unaangalia mahitaji yako kwa mara ya mwisho kama yametiamia kabla ya kutuma maombi au kwenda kujiunga na chuo, hii itahusisha taarifa zako binafsi.

Hivyo, soma kwa mara ya mwisho kuona iwapo taarifa zote muhimu zinazohitajika umekamilisha na vigezo vingine ili iwe rahisi kupokelewa na chuo husika unaweza kumpa msaidizi kuangalia kile ulichokiandika.

 

Tulia fanya maandalizi ya safari

Iwapo utajiridhisha yote haya basi kazi itakuwa ni kwako kuhakikisha kuwa unatuma maombi yako kabla ya tarehe ya mwisho, au unaweza kuweka  taarifa zako vizuri ukazituma mwezi julai kabla ya tarehe 30.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles