29.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Mambo yanayombeba Magufuli uchaguzi 2020

 BAADA ya ngwe ya kwanza ya miaka mitano (2015-2020) ya Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli kumalizika ni dhahiri yapo mambo ambayo yanampa ahueni na kutembea kifua mbele katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Magufuli yupo kwenye mikutano ya kampeni za kuwania kuchaguliwa kipindi cha pili tangu kuzinduliwa Agosti 26, mwaka huu.

Uchaguzi mkuu wa urais, ubunge na udiwani utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu, ambapo Magufuli anachuana na wagombea wengine 14 katika nafasi ya urais kutoka vyama vya ACT Wazalendo, Chadema, Chauma, NCCR Mageuzi, CUF na Demokrasia Makini kwa kuvitaja vichache.

Tangu Novemba, mwaka 2015 serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani kumekuwa na mafanikio ambayo yanawapa kifua mbele ikiwamo utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa miundombinu barabara, meli, viwanja vya ndege, ununuzi wa ndege, umeme, kufanya operesheni ya vyeti feki, kupambana rushwa, dawa za kulevya na utoaji wa elimu bure kwa kutaja machache.

Ni mafanikio gani aliyopata kwa miaka mitano? Uongozi wake katika kipindi cha miaka mitano, Rais Magufuli ameonesha uthubutu na mabadiliko katika maeneo kadhaa ambayo duru za kisiasa zinabainisha kuwa huenda baadhi ya wapigakura wapya kati ya milioni saba wakavutiwa mafanikio aliyopata kwa miaka mitano.

Mosi, kuvunja mifupa migumu; Magufuli ameonesha uwezo mkubwa wa kuchukua uamuzi mgumu ikiwamo kutekeleza mipango iliyokuwa imeshindikana takribani miaka 40 iliyopita.

Mojawapo ni kutekeleza mipango iliyopitishwa katika serikali ya awamu ya kwanza chini ya Julius Nyerere kuhamisha makao makuu ya nchi kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma. Halmashauri Kuu ya TANU (sasa CCM) ilipitisha mpango wa kuhamia Dodoma, lakini serikali hiyo haikuweza kutekeleza hadi ilipoondoka madarakani mwaka 1984 haikukamilisha. Serikali ya awamu ya tatu ya Rais Mkapa ilihamisha Wizara ya Kilimo na Ushirika jijini Dodoma lakini haikudumu huko, baadaye zilirejeshwa Dar es Salaam.

Pili, uamuzi wa kutekeleza mpango wa mradi wa umeme wa Bonde la Mto Rufiji nao umetajwa kuwa ni mafanikio kwa serikali ya Dk. Magufuli. Mradi huo umesuasua kwa miaka mingi tangu utawala wa awamu ya kwanza wa Mwalimu Nyerere, pamoja 

 na kukumbana na changamoto wataalamu wa mazingira lakini rais huyo ameshikilia msimamo wa serikali yake kujenga mradi wa umeme na ndiyo siri ya awamu ya tano.

Tatu, miradi ya kiuchumi: Mosi, sera ya viwanda SIDP (Sustainable Industrial Development Policy) ya mwaka 1996 inabainisha kuwa Tanzania hadi mwaka 2015 ilitakiwa kuwa na viwanda vya kati.

Sera hiyo ilipitishwa na serikali ya awamu ya tatu ya serikali ya Hayati Benjamin Mkapa na waziri wa viwanda na biashara wa wakati huo marehemu Dk. Abdallah Kigoda.

Hata hivyo, sera ya viwanda imepigiwa upatu na serikali ya awamu ya tano tangu kuingia madarakani. Serikali imefanya jitihada kuvutia wawekezaji na kusisitiza ujenzi wa viwanda kwa wadau mbalimbali wa uzalishaji, biashara na uchumi.

Nne, kuanzishwa vitambulisho vya machinga; Mwaka 2003 Profesa Hernando de Soto aliyekuwa mshauri wa serikali ya awamu ya tatu ya rais Benjamin Mkapa alipendekeza serikalini kuanzishwa mpango wa MKURABITA, ambapo ulibainisha umuhimu wa kurasimisha biashara zisizo rasmi mfano Mama Lishe, saluni, wamachinga na wafanyabiashara wengine wenye mitaji ya chini ya milioni moja.

Serikali ya awamu ya tano imetumia mpango huo vizuri na kupata mafanikio kwa kusajili vijana wengi waliojihusisha na biashara ya umachinga. Uongozi wake umerasimisha shughuli za wamachinga na Mama Lishe, pamoja na wajasiriamali wadogo kwa kutengeneza vitambulisho vya kuwatambua. Kundi hili linatajwa na wataalamu wa uchumi na siasa kwamba limebeba matumaini ya CCM kupata kura za ushindi katika uchaguzi ujao.

Tano, ununuzi wa ndege; Kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya 2015-2020 imeelezea suala la matengenezo ya viwanja na kufufua Shirika la Ndege (ATCL). Jumla ya ndege 11 zimenunuliwa na mamlaka za Tanzania. Hili ni eneo jingine linalotarajiwa kumwongezea wapigakura Rais Dk. Magufuli wakati wa kampeni. Matarajio ni ndege hizo kuongeza kiwango cha biashara ya utalii nchini humo pamoja na shughuli zingine za kiuchumi.

Sita, sekta ya afya; mpango wa kuongeza vituo vya kutoa huduma za matibabu ya magonjwa kama vile saratani kwenye hospitali za rufaa, pamoja na Kanda kama vile ya Ziwa ambayo kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, kanda hiyo ina watu wengi na inahitajika kuongezwa huduma 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,701FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles