24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mambo yamenoga Yanga

Winfrida Mtoi, Dar es Salaam

KLABU ya Yanga imeamua kufanya kweli kwa makocha wao baada ya kuwapa mkataba wa miezi 18, kocha mkuu Luc Eymael na msaidizi wake Riedoh Berdien.

Mkataba huo utawafanya makocha hao kuutumikia msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliobaki na ujao.

Eymael raia wa nchini Ubelgiji, alitua nchini wiki iliyopita na kuishuudia Yanga SC ikiondolewa na Mtibwa Sugar katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, wakati Berdien wa Afrika Kusini aliwasili juzi jioni.

Berdien aliyejiunga na Wanajangwani hao kwa mapendekezo ya Eymael, atakuwa kocha msaidizi na pia ni mwalimu wa viungo ambayo ndiyo taaluma yake.

Makocha hao walianza rasmi kukinoa kikosi hicho juzi kabla ya kuasani mkataba, huku wakishudiwa na mabosi wa Yanga kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema Kamati ya Utendaji imefikia makubaliano ya kuingia mkataba huo baada ya kuridhishwa na uwezo wao.

Alisema uongozi una imani kuwa makocha hao watawafikisha Yanga katika malengo waliyojiwekea ikiwamo kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mwakalebela alisema hamasa ya Wanayanga  ambayo Eymael aliona Zanzibar  na historia ya klabu hiyo ni moja ya vitu vilivyomfanya  akubali kusaini mkataba na wanaamini atakaa kwa muda mrefu zaidi mara baada ya mkataba wa sasa kumalizika.

“Watu wanasema  kocha huyu hakai muda mrefu, lakini wajue timu alizopitia hazina historia kubwa kama Yanga, pia alipofika Zanzibar  siku ya kwanza, aliona jinsi gani watu wa Yanga walivyokuwa na hamasa na timu yao, hii ni itakuwa moja ya sababu moja wapo ya kudumu naye na kufanya vizuri,” alisema Mwakalebela.

“Kuchukua ubingwa si kazi rahisi, tulihudhuria mazoezi ya kwanza ya mwalimu na viongozi wote, lengo lilikua kuona kwa vitendo ubora wa makocha hao ukiachana na CV, tumeona wanafaa sana,” aliongeza.

Kwa upande wake Eymael, alisema atafanya kazi yake kwa umakini mkubwa kuhakikisha timu hiyo inakuwa ya ushindani ndani na nje ya Tanzania.

“Nimewaona wachezaji wote ni wazuri na wanajituma mazoezini, kitu kikubwa cha kufanyia kazi ni kuwafanya waendane na falsafa yangu, napenda soka lakuburudisha, hivyo mashabiki wajiandae

“Roma haikujengwa kwa siku moja, lakini tutahakikisha tunapambana ili kuifanya Yanga iwafurahishe mashabiki hasa kwa aina ya uchezaji pamoja na kushinda na Simba SC na Azam FC kwenye kuwania mataji

“Nina uzoefu na soka la kiafrika, nimekaa Afrika Mashariki hivyo sioni kama kutakuwa na tatizo,” alisema Eymael.

Naye Berdien alisema anaijua Tanzania na amekuwa akifuatilia soka lake na moja ya timu kubwa ni Yanga, atatumia taaluma na uzoefu wake kuwaweka fiti wachezaji.

Berdien amefanya kazi na timu mbalimbali za Afrika kama vile Free State, Chippa United, timu ya Taifa ya Botswana, Bangladesh, Uganda na Afrika Kusinu ya Wanawake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles