24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MAMBO YA KUEPUKA PINDI MTOTO ANAPOUGUA KIFAFA

 

Na MWANDISHI WETU

KIFAFA ni ugonjwa unaosabababishwa na seli za mishipa ya fahamu zilizopo kwenye ubongo kutoa umeme [impulses] mwingi kuliko kawaida kwenda kwenye misuli na sehemu zingine za mwili. Matokeo yake mtu huanza kupata degedege mwili mzima, kukakamaa, kuanguka chini na kupoteza fahamu.

Mwaka 2013 ugonjwa huu uliua zaidi ya watu laki moja duniani, Asilimia 80 wakiwa Waafrika.

Mgonjwa wa kifafa anaweza kuanguka mara kadhaa kwa mwezi lakini pia anaweza asianguke kabisa iwapo atafuata masharti na utaratibu mzuri wa matibabu.

Mtu anapotaka kuugua kifafa anaweza kuhisi mwili unasisimka isivyo kawaida, misuli kuvutika/kukaza yenyewe na hata kupoteza fahamu.

Baadhi ya vifafa huwa ni matokeo ya magojwa mengine mwilini, kama upungufu wa sukari kwenye damu, kuumia kichwa, ajali za barabarani au kutumia dawa za kulevya kupita kiasi.

Ugonjwa huu pia unaweza kusababishwa na uvimbe kwenye ubongo ama tatizo lingine la afya linaloathiri ubongo.

Watoto walio chini ya miaka mitano huwa wanapata hali ya kifafa pale joto lao la mwili linapozidi nyuzi joto 38 (100.4° F (38° C) aina hii ya kifafa huitwa Febrile Seizure.

Unaweza kuogopa hali hii kama mzazi lakini huwa ni ya dakika chache tu na ni nadra kusababisha matatizo makubwa.

Kwa watoto chini ya miaka mitano, kushikilia pumzi kunaweza kusababisha hali ya kifafa, mfano kuna baadhi ya watoto pindi wanapokasirika huwa wanashikilia pumzi (hawavuti pumzi kwa sekunde chache) kabla tu ya kuachia kilio kikubwa.

Kabla ya kupoteza fahamu kifafa hufuatia… mara nyingi hali hii huisha yenyewe.

 

Kwa watoto wenye umri wa miaka mitano baadhi yao hukumbwa na hali hii lakini mara nyingi huisha baada ya sekunde chache.

 

Fanya hivi kwa mtoto

Kama mtoto wako amepatwa na kifafa, unashauriwa kumlaza chini upande wake wa kulia katika sehemu ambayo ni salama.

Pia hakikisha unaondoa kitu chochote cha hatari kilichopo karibu kama chupa, chuma, sindano, mawe, mvue cheni shingoni kama alivaa, mvue nguo iwapo ipo shingoni ili kuepuka kumkaba.

Usijaribu kupanua mdomo wa mtoto anapokuwa na kifafa ama kuweka kitu mdomoni kwake, pia usijaribu kuzuia kuweweseka kwake.

Mara tu kifafa kinapoisha, mfariji mtoto. Ni muhimu kwa watoto kuendelea kulala chini mpaka hali hii itakapoisha kabisa, subiri hadi yeye mwenyewe atake kuinuka.

Unashauriwa kumwita daktari iwapo kifafa kitaendelea zaidi ya dakika tano, pia kama atashindwa kupumua.

Ni vyema kutambua kuwa mara baada ya mtoto kutoka kwenye hali hii huwa anakuwa amechoka na akili yake huvurugika, hali ambayo inaweza kumfanya alale usingizi mzito. Ukiona hali hiyo hupaswi kumwamsha wala kumpatia chakula hadi pale atakapoamka. Jambo la kuzingatia ni kuhakikisha anapata hewa ya kutosha na anapumua vizuri.

Mara baada ya usingizi kuisha, unaweza kumtaarifu daktari kwa ajili ya kuja kuangalia kilichosababisha mtoto kukumbwa na hali hiyo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles