23.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

MAMBO MATANO YANAYOWEZA KUHARIBU AFYA YAKO

Na MWANDISHI WETU,

KUNA baadhi ya mambo ambayo mara nyingi ukiyafanya huwa ni lazima ufupishe maisha yako kwa namna moja au nyingine. Hii yote huwa inatokana na aina ya maisha uliyoyachagua, ambayo huwa ni hatari kwa afya na maisha kwa ujumla. Watu wengi wana tatizo la kuishi maisha ya kujisahau na kufanya vitu ambavyo ni hatari. Haya ni baadhi ya mambo ambayo ukipendelea kuyafanya basi maisha yako yanakuwa hatarini.

Kula bila mpangilio

Watu wengi huwa wanaishi maisha ya kutojali afya zao. Yapo mambo ambayo ukiyafanya afya yako inakuwa hatarini moja kwa moja hata kama hujasomea udaktari ni rahisi kwako kuyafahamu.

Mfano kama unapenda kula vyakula bila mpangilio na vibovu ambavyo havifai, ni lazima afya yako itakuwa hatarini. Lakini si hivyo tu, kama wewe ni mvutaji mzuri wa sigara au unakunywa pombe kupita kiasi bila utaratibu, ni rahisi mno kwako kuweza kuharibia afya yako na hivyo kuyafanya maisha yako kuwa hatarini.

Maisha ya upweke

Hakuna kitu hatari katika maisha yako kama kuamua kuishi wewe kama wewe. Hili ni jambo la hatari mno kwako na kwa namna yoyote ile linaweza kuhatarisha afya yako. Kwa kawaida binadamu ameumbwa ili kuweza kuwa na uhusiano na wengine. Sasa wapo watu ambao hawana uhusiano mzuri na wengine kwa sehemu kubwa.

Watu hawa kutokana na kutokujihusisha kwao na watu wengine hujikuta wakiwa na  maisha magumu. Muda mwingi mawazo yao huwa ni hasi kutokana na kujitenga na hivyo hujikuta ni watu wa kuwa na msongo wa mawazo, hivyo huwa ni rahisi kwao kupoteza maisha.

Kukaa chini muda mrefu

Hili ni jambo dogo tu, na unaweza ukalichukulia kwa urahisi, lakini wataalamu wa afya wanaonya jambo hili kwa kuwa linaweza kuathiri afya. Inashauriwa kuwa si vizuri kukaa chini kwa muda mrefu bila ya kusimama. Hiyo inaweza kukusababishia magonjwa kadhaa ikiwamo uti wa mgongo.

Ili kuweza kulinda afya yako na kuwa bora zaidi unapaswa kuepuka kukaa chini kwa muda mrefu. Kama una kazi ambayo inakulazimu ukae chini muda mrefu basi jitahidini angalau uwe unasimama kila baada ya dakika 45 ili kufanya mzunguko wa damu uendelee vizuri.

Kuangalia runinga kwa muda mrefu

Wataalamu wa afya wanabainisha kuwa kuangalia TV kwa muda mrefu tena ukiwa karibu nayo unaweza kuua baadhi ya seli ndani ya mwili. Kwa upande wa wanaume tafiti zinaonyesha kuwa kuangalia TV kwa muda mrefu hupunguza uwezekano wa kuzalisha mbegu za kiume kwa asilimia kubwa.  

Kikubwa cha kuzingatia hapa ni kutambua kuwa kuangalia runinga kwa muda mrefu kwa namna moja au nyingine kuna madhara ambayo unaweza usiyaone kwa urahisi.

Kutopata usingizi wa kutosha

Kukosa usingizi ni tatizo ambalo linaiweka afya yako hatarini moja kwa moja. Kwa kawaida binadamu anatakiwa alale saa 8 kwa siku. Unapokosa kulala saa hizo unaweza kupoteza kumbukumbu taratibu.

Lakini si hivyo tu, pia hukusababishia kupata tatizo la akili. Kwa hiyo, usingizi ni jambo muhimu mno kwa afya yako.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles