31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MAMBO 7 AMBAYO MARA CHACHE UTAAMBIWA AU KUYASIKIA KUHUSU MAHUSIANO/NDOA

Na Dk. Chris Mauki


  • YAMKINI ipo siku utaamka katikati ya usiku wa manane na kumtazama aliyelala pembeni yako (ambaye labda unamuita au anajiita mpenzi wako) na kujiuliza “hivi maisha haya na huyu mtu ndo hadi kifo kweli?”(ukitamani walau kuwepo na kaupenyo kakutokea).

Swali hili linasababishwa na aina ya maisha mnayoishi, yamkini penzi mlilokuwa nalo awali haulioni au wote hamlioni tena, imebaki kuonekana tu na watu wa nje kama mnaopendana kumbe ukweli ni kwamba mnaishi tu pamoja “not as lovers but as in mates”.

Zile zama za kuitwa jina lako la kwanza, na yale majina mengine kama darling, honey, sweet heart zimefia mbali na nafasi yake imechukuliwa na majina kama ‘mama nanihii’ baba naniii’ we nanihii’ eti nanihii’ eti wewe’!!! Ile “chemistry” au ule mvuto wa ndani ambao ulikuwa unausikia kutokea moyoni hadi katika mifupa yako mtu huyo akiwa karibu nawewe hauioni tena badala yake, akiwepo karibu ndio unaona bora awe mbali. Kipindi hiki mtu huyu akisafiri hutamani arudi, kila siku unamuuliza “unarudi lini eti?” sio kwa kusukumwa na hamu ya kutaka arudi mapema bali kwa kusukumwa na hamu ya kutaka kusikia yamkini kaongeza siku au amepata safari nyingine ya gafla ili uendelee kufurahia kutokuwepo kwake.

  • Maranyingine utajikuta inakulazimu kufanya kazi ya ziada kuliko uliyowahi kudhania katika kuhakikisha penzi lenu linasonga

Yamkini ulifikiri kuwa itakuwa rahisi mara ukikubali kuingia kwenye mahusiano na huyo mpenzi wako. Umetamani kuwa nae kwa muda, umemtafuta kwa muda na sasa ukafikiri mkiamua kuanza mapenzi pamoja ‘things will go smooth’.

Mnakuja kugundua kuwa ninyi ni watu wawili tofauti, kila unachokipenda na kukitamani mwenzako hakithamini. Yale uliyokuwa ukiyaamini kama misingi ya mahusiano bora huyaoni kwenye mahusiano yako.

Kila ulichowahi kukisoma, kujifunza au kuambiwa kuhusu kuyafanya mahusiano yawe paradiso unaona hakifanyi kazi kwenu.

Matarajio yako makubwa kwenye mahusiano yenu na mustakabali wenu yanaingia ukungu na mbele yako huoni hata chembe ya mwanga.

Sasa unajikuta ulichodhania ni rahisi kumbe sio, na unalazimika kujituma zaidi, kufanya kazi zaidi na kutumia muda yamkini kuliko mwenzako kuhakikisha mnaweka sawa mambo yenu ili angalau maisha yaendelee.

Kuepuka hili nivema tunapoingia katika mahusiano tusiwe na matarajio makubwa kupitiliza na yasiyo tekelezeka “overambitious and unrealistic expectation” Penzi peke yake ndilo litupeleke katika mahusiano kwa kiu ya kusaidiana kuhakikisha raha ya kilammoja inawezeshwa, sio kwa kiu ya kutimiziwa kiu zako tu ‘this is ultimate selfishness’.

  • Zipo nyakati unaweza kujikuta unaenda kitandani ukiwa na hasira, na yamkini ukaamka asubuhi ukiwa na hasira zaidi ya ulizo lala nazo.

Tofauti baina ya jinsia hizi mbili kama nilivyogusia kwenye jambo la pili ziko katika maeneo mbali mbali ya mahusiano yetu na mojawapo ni tofauti tulizonazo baina ya wanawake na wanaume hususani katika kuishuhulikia migogoro inayoibuka ndani ya mahusiano yetu.

Yawezekana wewe ni mmoja wa wale wasio na hasira sana, muelewa, mwepesi wa kusamehe na kuchukuliana na hali, mara kwa mara unatamani mliongee jambo lililoleta utata baina yenu kabla halijakuwa kubwa na kuleta madhara. Tabia hii ni nzuri sana, lakini kwa bahati mbaya unakutana na mwenzako ambaye hakufunzwa vyema namna na jinsi ya kuishuhulikia migogoro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles