24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 29, 2023

Contact us: [email protected]

Mama wa Mtanzania aliyehukumiwa maisha Kenya kwa ugaidi afunguka

Upendo Mosha- Same

MAMA mzazi wa Mtanzania Rashid Mberesero, aliyehukumiwa kifungo cha maisha jela nchini Kenya, baada ya kukutwa na hatia ya kufanya shambulio la kigaidi eneo la Garissa  na  kusababisha vifo vya wanafunzi 148, amevunja ukimya.

Mberesero ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha huku wenzake Hassan Edin na Mohamned Ali Abikar kila mmoja akihukumiwa miaka 41 gerezani, walipatikana na hatia ya kupanga shambulio hilo chini ya ushirikiano wa kundi la Al-Shabaab.

Akizungumza na MTANZANIA, Fatma Ally ambaye ni mama mzazi wa Mberesero, alisema kutokana na hukumu iliyotolewa anamwachia Mungu.

Hata hivyo, aliomba msaada wa mashirika mbalimbali na taasisi zinazojihusisha na masuala ya kisheria kumsaidia mwanawe kupunguziwa adhabu.

“Tangu hukumu ya mwanangu kutolewa, hali yangu ya kiafya si nzuri, zaidi sana namwachia Mungu maana yeye ndiye hakimu wa kweli, lakini pia naomba kama kuna uwezekano wa kujitokeza taasisi au watu wanaojua masuala ya sheria, wamsaidie walau apunguziwe adhabu,” alisema.

Aidha alisema tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa kwa kipindi cha miaka minne, hakubahatika hata mara moja kuhudhuria mahakamani kutokana na hali ngumu ya maisha inayomkabili jambo ambalo lilimfanya kutojua kitu kinachoendelea.

“Tangu kesi hii ianze ni miaka minne sasa na sijwahi kufika mahakamani kusikiliza, hata siku ya hukumu sikuweza kwenda kwa sababu sina uwezo wa kupata nauli ya kutoka huku kijijini hadi huko Kenya,” alisema.

Mberesero aligundulika eneo la tukio akiwa si mwanafunzi wala mfanyakazi wa chuo hicho.

Kulingana taarifa zilizoripotiwa, Mberesero aliyesoma Shule ya Bihawana mjini Dodoma, alidaiwa kutoroka shule baada ya kukatazwa kuvaa kofia.

Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo wakati huo, Mberesero alijiunga mwaka 2015 baada ya kutoka Shule ya Bahi Kagwe.

Cha kushangaza ni kwamba licha ya kutoweka shule, hakuna aliyefuatilia alikokwenda.

Kwa takriban miezi minne wazazi wa kijana huyo walidhani mtoto wao yupo shule suala ambalo halikuwa la kweli.

Hata hivyo, wazazi walishangaa kugundua mtoto wao alikuwa miongoni mwa waliopanga na kutekeleza shambulio la Garissa.

Kwa takriban miezi minne, wazazi wa kijana huyo walidhani kwamba mtoto wao yupo shule suala ambalo halikuwa la kweli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,259FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles