25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mama wa kambo jela kwa kumlisha mtoto hedhi

KAMPALA, UGANDA

MWANAMKE wa nchini Uganda, Annet Namatawa mwanamke amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kumlisha binti yake wa kambo damu ya hedhi.

Mwanamke huyo amekiri kosa hilo mbele ya mahakama na akaomba msamaha kwa madai kuwa yeye ni mama wa watoto watatu.

Gazeti la nchini Uganda la Daily Monitor limeripoti kuwa hakimu katika mahakama ya Mukono alimpunguzia kifungo Annet kutoka  miaka saba hadi miaka miwili kwa sababu mwanamke huyo aliisaidia mahakama kwa kutopoteza muda wake kwa kukiri kosa.

Taarifa ya hukumu dhidi ya Annet  imeibua hisia kali miongoni mwa Waganda huku wengine wakijiuliza ni vipi aliamua kutekeleza kitendo hicho.

Annet anadaiwa kumlisha binti yake wa kambo damu ya hedhi miezi mitatu iliyopita katika kijiji cha Kitega kilichoko kilomita 46 (maili 28 ) mashariki mwa mji mkuu wa Uganda, Kampala.

Mume wake anaripotiwa kutofurahishwa na hukumu iliyotolewa na alitaka mke wake afungwe kwa muda mrefu zaidi.

Gazeti la Uganda la Observer mwezi uliopita liliripoti kwamba mwanamke huyo alikabidhiwa kwa polisi na mume wake ambaye alifahamishwa tukio hilo la wanakijiji.

Inaripotiwa kuwa Annet alichanganya damu ya hedhi na chakula na baadae kumlisha binti yake wa kambo.

Vyombo vya habari pia vimeripoti kuwa mwanamke huyo pia amekiri kuwa alimlisha mtoto huyo damu ya hedhi kutokana na hasira iliyosababishwa na jinsi mume wake anavyomdekeza mtoto huyo.

“Hukumu hii itawashawishi wanawake wengine kufanya sawa na aliyoyafanya huyu wakijua kuwa hukumu yake sio nzito ,” alisema Susan Mayanja ambaye ni Katibu wa Kijiji cha Kitega.

Aliwashauri wanawake kuwalea watoto wa kambo kwa upendo kwasababu hawajui hali yao katika siku za baadae.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles