25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mama Sitta: Vyeo vya kisiasa sio mbadala wa ndoa

Mwandishi wetu, Dodoma

Wanawake wanasiasa wametakiwa kutofanya vyeo vyao kama mbadala wa ndoa na badala yake waendelee kulinda ndoa zao na kuzipa umuhimu wake.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), Margreth Sitta alipokuwa akizungumza katika mkutano kati ya wabunge na Mtandao wa Ushiriki Tanzania unaosimamia  ushiriki wa kisiasa wa wanawake, vijana na wenye ulemavu.

Katika mkutano huo Mama Sita ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Waziri wa Elimu alisema  wanawake  wanatakiwa wajue kuwa kugombea ni muhimu lakini ndoa nayo ni muhimu.

“Tukitoa elimu hii itasaidia wanaume wasiogope kuwaachia wanawake kugombea nafasi mbalimbali kwani tabia hizo ndizo zinazofanya wanaume wawazuie wanawake kushiriki siasa.

“Niliwahi kusema mume wangu alikuwa ni mwanaume wa msimamo, ni muhimu kujua wakati gani umuendee kumueleza, tenga muda sahihi wa mume wako, ujue wakati wa kumueleza jambo lako lakini pia unatakiwa ujue hauwezi kushika madaraka wakati ukirudi nyumbani unapigana na mume, ni lazima hali iwe nzuri nyumbani.

“Wanawake tunapopata madaraka haya, tuendelee kulinda yale majukumu yetu ya nyumbani sio kwa sababu umekuwa kiongozi hata kupika hupiki, mume wako hali chakula chako tena, kingine ni kumjua mume uliye naye na namna ya kumshirikisha,” ,” amesema mama Sitta.

Kwa upande wake Mbunge wa Chadema, Susan Lymo, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wanawake alisema wabunge walio majimboni wanatakiwa wafanye jambo ili kuwahamasisha ambao hawamo.

“Nimefurahi kuwa Ushiriki Tanzania imeziunganisha taasisi zote 23 zenye mrengo huu, kwani umoja ni nguvu, lakini tunatakiwa kujua namna ya kuwahamasisha wanawake katika hili,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles