23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Mama Ongea na Mwanao kugawa viatu vya shule kwa watoto

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao inatarajia kuanza kampeni ya kugawa viatu vya shule kwa watoto wa shule za msingi nchi nzima ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha elimu.

Akizungumza Dar es Salaam Septemba 14, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Steven Mengele amesema wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kijamii ili kusaidia juhudi za Serikali.

Amesema wanatarajia zoezi hilo kuanza kwa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ambapo lengo ni kufikia mikoa yote nchini.

“Zoezi hili tutalifanya nchi nzima tumelenga vijijini na tutalifanya wenyewe na si kukabidhi kwa uongozi wa shule kwani lengo letu kuhakikisha vinamfikia mlengwa,” amesema Steven.

Amesema Serikali ya awamu ya sita imeweka miundombinu mizuri katika sekta ya elimu hivyo wanawajibu kama taasisi inayounga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dk. Samia kuhakikisha watoto wanaipenda shule.

“Miundombinu imeboresha sana sasa tunataka huyu mtoto aipende shule watoto wengi vijijini wamekuwa wakienda shule peku au na malapa hii hali inapelekea mtoto akichomwa tu miba njiani kesho hataki tena kurudi shule,” amesema Mengele.

Mengele ametoa wito kwa viongozi wote wa mikoa watakayopita kutoa ushirikiano ili zoezi Hilo liweze kufanikiwa na wadau wanaweza kuchangia chochote kwa sababu kuna changamoto nyingi mashuleni.

Kampeni hiyo ikianza mwaka jana ambapo waligawa zaidi ya viatu 2,000 kwa watoto katika mkoa ya pwani wilaya ya Kibiti na mkoa wa Tabora na wilaya zake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles