24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Mama na mtoto wake wauawa kikatili

Arusha Town
Arusha Town

Na Eliya Mbonea, Arusha

MKAZI wa eneo la Baraa Ngulelo, jijini Arusha, Lightness Thomas na mtoto wake wa kike, Joyna Charles (9), wamekutwa wamekufa ndani ya nyumba yao huku vichwa vyao vikiwa vimetobolewa na kitu chenye ncha kali.

Miili ya watu hao iligundulika ndani ya nyumba yao usiku wa Julai 27, mwaka huu, kitandani na kufunikwa blanketi, huku ikiwa imeharibika vibaya.

Akizungumza na MTANZANIA, ndugu wa marehemu ambaye hakupenda jina lake litajwe kwenye gazeti, alidai watu hao walifanya mauaji hayo usiku wa Julai 23, mwaka huu.

“Julai 24 baadhi ya ndugu na rafiki zake walikuwa wakimtafuta kwenye simu bila kumpata na kuanzia wakati huo hadi Julai 27, mwaka huu ndipo walipobaini miili yao ikiwa ndani,” alisema ndugu huyo wa marehemu.

Akifafanua kuhusu namna walivyoikuta miili hiyo, alisema wakiwa na askari polisi, mwenye nyumba na daktari pamoja na majirani walilazimika kuvunja mlango wa nje na wa chumbani kutokana na mtu aliyefanya mauji hayo kufunga milango yote na kuondoka na ufunguo.

“Tukiwa pale nyumbani hatukuamini haraka kama ameuawa, japo kulikuwa na hewa nzito kwa nje,” alisema ndugu huyo.

Alisema baada ya kuingia ndani waliwakuta marehemu hao wakiwa wamelazwa kitandani huku wamefunikiwa blanketi.

“Marehemu wote wawili walikuwa wamevimba sana lakini vichwani walionekana kuwa na majeraha ya kupigwa na vitu vyenye nchi kali, kutokana na hali hiyo askari polisi pamoja na majirani tulisaidiana kwa pamoja kwa kuichukua miili hiyo na kuipelekea Hospitali ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi,” alisema.

Kutokana na tukio hilo la mauaji, MTANZANIA lilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, ambapo muda wote hakupatikana ofisini kwake wala kwenye simu yake ya kiganjani.

Miili hiyo ya marehemu hao ilisafirishwa juzi kwa ajili ya maziko nyumbani kwao, wilayani Karatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles