21.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Mama mzazi wa Kabendera afariki dunia

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MAMA mzazi wa mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera ambaye kwa sasa yuko rumande katika gereza la Segerea amefariki dunia.

Verdiana Mjwahuzi (80), alifariki dunia jana Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu na baadaye mwili wake kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Rufaa Amana.

Kabendera alikamatwa Julai 2019 akikabiliwa na makosa kadhaa ikiwamo utakatishaji fedha, kukwepa kodi na kushiriki katika genge la uhalifu.

Akizungumza jana, Almachus Kabendera ambaye ni baba mdogo wa Kabendera, alisema baada ya kutokea msiba huo ulifanyika mchakato wa kufikisha taarifa kwa mtoto wake ambaye yupo mahabusi katika gereza la Segerea na kwamba alipokea kwa masikitiko taarifa za kifo hicho.

Almachus alisema Kabendera alipofikishiwa taarifa hizo alijawa na huzuni na kuanza kububujikwa na machozi.

“Nafikiri unajua msiba wa mzazi uanavyoshtua, kwani hata naye (Kabendera), alipokea kwa mshtuko taarifa za msiba… tulijitahidi kuzungumza naye na kumweka sawa na kwa sasa tunaendelea na taratibu za mazishi,” alisema Almachus.

Alipoulizwa kuhusu ratiba ya msiba, alisema kuwa wanatarajia kuaga mwili wa marehemu Ijumaa na baada ya hapo baadhi ya ndugu wataanza safari ya kuelekea mkoani Kagera huku mwili ukitarajiwa kusafirishwa Januari 4, kwa ndege.

Alisema mazishi  yatafanyika Januari 6 katika Kijiji cha Katoma, Wilaya ya Bukoba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,717FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles