23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

MAMA ATAKIWA KUTHIBITISHA KAMA KWELI ANANYONYESHA

Na MWANDISHI WETU,

MWANAMKE mmoja amewasilisha malalamiko yake kwa maafisa wa polisi wa Ujerumani, akidai kudhalilishwa baada ya kuambiwa atoe maziwa yake katika eneo la usalama la uwanja wa ndege.

Amri hiyo alipewa na maafisa wa polisi wa uwanja wa ndege wa Frankfurt waliotaka kuthibitisha kama kweli ananyonyesha mtoto.

Mama huyo aliyejulikana kwa jina la Gayathiri Bose, alisema kuwa alifedheheshwa kupita kiasi hivyo ana mpango wa kuwasilisha malalamishi yake rasmi mahakamani.

Alisema maafisa wa polisi hao walimtuhumu kwamba alikuwa amebeba pampu ya kutoa maziwa licha ya kwamba hakuwa na mtoto.

Hata hivyo, polisi wa Ujerumani wamekataa kutoa tamko lolote kuhusu madai hayo na kusema kwamba hatua hiyo si ya kila siku.

Bose ambaye alikuwa akisafiri pekee alisema wakati akiwa anaelekea kupanda ndege kuelekea Paris, Ufaransa wiki iliyopita, alipofika katika sehemu ya kukaguliwa kiusalama alisimamishwa na kuanza kuhojiwa.

Mwanamke huyo aliyekuwa akitokea Singapore, alisema alianza kuhojiwa baada ya kukutwa na pampu ya kukamulia maziwa ndani ya mkoba wake.

“Je, unanyonyesha? Basi mtoto yuko wapi? Mwanao yuko Singapore?” aliulizwa na maafisa hao wa polisi.

Bose alisema kuwa maafisa hao hawakumuamini aliposema ana mtoto na kwamba kifaa hicho ni cha kukamulia mziwa.

“Walichukua pasipoti yangu na kuizuia… baadaye nikapelekwa katika chumba kimoja kwa ajili ya mahojiano zaidi.

''Ndani ya chumba hicho afisa huyo wa polisi alinitaka kuthibitisha kuwa ninanyonyesha na kutoa maziwa.

''…Niliwaaambia kwamba hakuna kitu kama hicho, sisi huweka pampu hiyo katika matiti yetu na mashine hufanya kazi hiyo,” alisema mama huyo na kuongeza:

“Alitaka nikamue maziwa ili aone kama kweli nanyonyesha.”

Bi Bose alisema alikubali kufanya hivyo akafinya matiti yake, licha ya kwamba alishangazwa na hatua hiyo.

''Nilikuwa peke yangu na sikujua ni nini kitafanyika iwapo watataka kunilaumu. Nilipotoka katika chumba hicho ndipo nilipoelewa kile kilichokuwa kikitendeka, kabla ya hapo nilidhani kama masihara,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles