28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mama aenda na polisi kumchukua mwanae aliyechanganywa na pacha Kenya

Na MWANDISHI WETU

HALI ya taflani iliibuka jana baada ya Angeline Omina ambaye ni mama wa msichana aliyelelewa pamoja na mmoja wa pacha waliochanganywa kwenda kumchukua  kwa nguvu  mwanawe, Mevis Imbaya.

Tukio hilo  limekuja baada ya siku chache mamlaka za nchini Kenya kutegua kitendawili cha pacha Sharon Mathius na Melon Lutenyo kufanana licha ya  kutoka familia mbili tofauti 

Matokeo ya vinasaba ambavyo vinaonyesha pacha hao ni ndugu kwa asilimia 99.9 yalikuja baada ya gumzo kutawala mitandaoni. 

Msichana wa tatu Melvis Mbaya, ambaye alikuwa akilelewa na pacha mmoja wapo matokeo hayo yalionyesha si ndugu yao halisi wa kuzaliwa na hivyo kujenga hisia kwamba walichanganywa hospitalini miaka 19 iliyopita wakati walipozaliwa.

Omina ambaye ni mfanyabiashra ndogo ndogo  wa Kangemi, Nairobi alikuwa amefuatana na maofisa watatu wa polisi wakati alipofika kumchukua mwanaye Mevis.

Huku akiwa amekasirika Omina aliishutumu familia ya mapacha hao kwa kumlazimisha binti yake, Mevis, kuendelea kuishi na Rosemary Onyango, ambaye ni mama wa mapacha hao na ambaye tangu akiwa kichanga nyumbani kwao Furfural, Kaunti ndogo ya Likuyani. 

“Siwezi kubaki bila mtoto. hilo haliwezi kutokea,” alisikika akisema Omina.

Inaelezwa Omina alianzisha taflani hiyo wakati binti yake, Mevis, pamoja na wasichana hao pacha, Sharon Mathius na Melon Lutenyo na jamaa zao wakijindaa kukutana na Gavana wa Kakamega, Wycliffe Oparanya. 

Omina aliwashutumu ndugu wa pacha hao kwa kumshinikiza binti yake Mevis kuendelea kuishi na Rosemary Onyango, mama wa pacha hao huko Fufural.

Kabla ya ripoti ya uchunguzi wa vinasaba (DNA) haijatoka wasichana hao walifanya uamuzi wa kuishi pamoja kama ndugu pasipo kushinikizwa.

Hata  hivyo Omina anasema amebaini kuna nia ovu inayofanywa upande wa pili na ndio sababu ya yeye kutaka kuondoka na mwanae.

Pacha hao Sharon Mathius na Melon Lutenyo ambao wote ni watahiniwa wa kidato cha nne  wamekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii 

baada ya picha zao kuonekana hadharani wakiwa wamefanana licha ya kutoka katika familia mbili tofauti.

Matokeo ya DNA yalionyesha kuwa mama  halisi wa pacha hao ni Rosemary Khaveleli Onyango wakibainika kuwa na chembechembe kwa asilimia 99.999.

Kwa mujibu wa matokeo hayo ya DNA hata hivyo yalionyesha Mevis ana chembechembe sawa kabisa na za Angeline Omina na Wilson Lutah Maruti yakithibitisha kwamba huyo ni mtoto wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles