23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

‘MALKIA MWEUSI’ AHAMASISHA WAAFRIKA KUPENDA RANGI YAO

HUYU ni mwanamitindo wa Sudan Kusini anayejivunia rangi ya ngozi yake nyeusi, ambaye anawaasa mabinti weusi kuona fahari ya rangi ya ngozi yao waliyobarikiwa na muumba

Mwamamitindo huyu, Nyakim Gatwech (24) maarufu Malkia Mweusi aliwahi kupewa na dereva teksi wa kampuni ya Uber ya pauni 10,000 za Uingereza sawa na Sh milioni 30 za Tanzania achubue rangi yake ili awe mweupe.

Kauli ya ofa hiyo ilimfanya ajawe na mshangao asiweze kujibu mara moja badala yake kuangua kicheko cha nguvu kabla ya kumjibu dereva teksi huyo mjinga: “Nawezaje kuharibu ngozi ya thamani kama hii?”

Nyakim, ambaye kwa sasa anaishi Minneapolis, Minnesota, nchini Marekani hutumia akaunti yake ya Instagram si tu kuonesha pozi mbalimbali za kimitindo bali pia kuhamasisha binti weusi kupenda rangi za ngozi zao.

Anandika katika Instagram: bila kujali kila aina ya maneno unayotupiwa kuhusu ngozi yako: unabakia bado mrembo na ninapenda kwa namna nilivyo.

“Unaniwakilisha nami nakuwakilisha na hivyo tuioneshe dunia namna tulivyo wazuri, warembo  na wenye akili mbali ya ngozi yetu nyeusi,” anaandika.

“Kwa sababu kuna maoni tofauti katika jamii kuhusu ngozi yetu nyeusi kwa wale wasioweza kupaza sauti kuitetea. Zungumza kwa wale wasioweza na bakia imara katika urembo wako huo.”

Katika ujumbe mwingine aliotupia mtandaoni, anasema: “Weusi ni ukakamavu, weusi ni uzuri, weusi ni dhahabu.”

Usiruhusu viwango vya Marekani viharibu roho yako ya Kiafrika. Penda ngozi yako bila kujali rangi wala kuibadili.”

Hata hivyo, ilimchukua muda kwa Nyakim kuwa na pendo alilo nalo sasa kwa ngozi yake mwenyewe baada ya kuzomewa, kuchekwa wakati akikua.

Kauli chafu kama vile ‘wewe mweusi kama jehanamu, mwenye ngozi iliyoungua, kaoge’, zilimfanya aichukie rangi yake hiyo na kufikiria kuondokana nayo.

“Kipindi hicho katika maisha yangu nilifikiria kujichubua ili kuondokana na mwonekano mbaya na vicheko na ili wavulana wanione mwenye mvuto,” alisema.

Lakini msaada aliopata kutoka kwa wafuasi katika mitandao ya jamii ambao katika Instagramu pekee wanafikia 154,000 kulimbadili na kuwa mwenye kujiamini.

Na dada yake pia alimsaidia mno kumfanya ajiamini na kujiona fahari kwa uzuri wa ngozi yake.

Mwisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles