25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, January 29, 2022

MALKIA ELIZABETH AANZA KUGAWA MAJUKUMU

LONDON, UINGEREZA


MALKIA Elizabeth II wa hapa, ambaye wiki iliyopita aliadhimisha miaka 91 ya kuzaliwa ameagiza wanafamilia wake wa kifalme kumwakilisha katika baadhi ya majukumu yake.

Kuna ripoti afya ya kiongozi huyo aliyezaliwa Aprili 21, 192 inaendelea kuzorota.

Kwa kawaida Malkia husherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa awamu mbili; Kwanza katika tarehe ambayo alizaliwa na katika sherehe rasmi ya mwezi Juni.

Hiyo ni kuendana na mila na utamaduni wa kale kwa lengo la kuepuka machafuko ya hali ya hewa.

Hivi karibuni wakati akiwa katika ziara Ireland Kaskazini,  Malkia Elizabeth alizungumzia afya yake akisema kuwa bado yu salama.

“Bado niko hai,” alisikika akitania Malkia huyo.

Malkia Elizabeth ndiye mtawala aliyeongoza muda mrefu zaidi katika historia ya Uingereza, akiwa amekaa miaka 64 madarakani.

Na amekuwa kwenye ndoa kwa kipindi cha miaka 68, akiwa ametembelea nchi 117 duniani na kufanya kazi na mawaziri wakuu 12 wa Uingereza.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
177,207FollowersFollow
532,000SubscribersSubscribe

Latest Articles