28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Malinzi asikitishwa matokeo Twiga Stars

malinziNA ELLY MHAGAMA, DAR ES SALAAM

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi, amesikitishwa na matokeo mabovu ambayo timu ya Twiga Stars inayapata katika michuano ya All African Games inayoendelea nchini Congo Brazzaville.

Malinzi alitoa kauli hiyo jana, akidai matokeo hayo mabovu yanatokana na kukosa ligi ya Taifa ya soka la wanawake, ambayo ingesaidia kuibua vipaji lukuki.

“Tunafungwa kwa sababu hakuna Ligi ya mchezo huu, tunatarajia kuanzisha Ligi ambayo tutazalisha wachezaji wapya,” alisema.

Twiga Stars juzi ilikubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Nigeria ‘Super Falcons’, katika mchezo wa Kundi A la michuano ya soka kwa wanawake.

Kipigo hicho ni cha pili kwa Twiga, baada ya mwanzo kukubali kufungwa bao 1-0 na Ivory Coast, hivyo kuishia hatua ya makundi.

Aidha, hii inakuwa mara ya pili Nigeria inaichapa Tanzania 3-0, baada ya mwaka 2010 kuifunga hivyo hivyo pia kwenye michezo hiyo hiyo ya Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles