27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Malinzi agusa suala la Niyonzima, Yanga

niyoADAM MKWEPU NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi, ameitaka klabu ya Yanga kukaa ili kumalizana na mchezaji Haruna Niyonzima, kama ikishindikana wapeleke kesi hiyo yenye mgogoro wa kimkataba kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji kabla ya wao kuingilia.

Hatua hiyo imekuja baada ya uongozi wa Yanga kuvunja mkataba wa mchezaji wake kiungo mkabaji, Haruna Niyonzima, kwa madai alikuwa akivunja utaratibu pamoja na kutaka kuwa juu ya klabu.

Katika uamuzi huo klabu ya Yanga ilimtaka mchezaji huyo kuilipa gharama ya mkataba huo dola 71,175 ambazo ni sawa na shilingi milioni 152.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Malinzi alisema bado Shirikisho hilo halijapata taarifa juu ya kuvunjwa kwa mkataba wa mchezaji huyo.

“Uongozi wa klabu pamoja na mchezaji wanatakiwa kuheshimu na kufuata utaratibu wa mikataba wanayowekeana  ili kuepuka  migongano.

“Kila klabu ina sheria zake, hivyo wachezaji wanatakiwa kufuata na kuheshimu taratibu ambazo klabu yake inataka pia kwa klabu nazo zinatakiwa  kufanya hivyo,” alisema.

Katika hatua nyingine, Malinzi aliwataka wasemaji wa klabu watumie vema nafasi zao wanazopewa na si kutumia nafasi hizo kwa mambo yao binafsi.

Hayo yamekuja mara baada ya Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro, kuzungumza maneno yaliyo nje ya klabu kwenye mkutano na waandishi wa habari.

“Unapokuwa umepewa mamlaka ya kusimamia kitu, unatakiwa kufuata kile kilichokuweka pale na sio kutumia nafasi hiyo kufanya mambo mengine kitu ambacho kinakuwa sio kizuri katika kazi,” alisema.

Hata hivyo, Malinzi alimtaka Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura pamoja na Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto, kuitisha semina ya wasemaji wa klabu ili kuwapa somo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles