27.7 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Malima”Ndolela” kutumbuiza siku ya kilele cha usalama barabarani

Na Oliver Oswald, Mtanzania Digital

Msanii mashughuri wa nyimbo za asili nchini, Malima Kabondo maarufu kama “Ndolela” anatarajiwa kutumbuiza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya usalama barabarani ambayo kitaifa yatafanyika Machi 14, mwaka huu, mkoani Mwanza.

Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya ‘Tanzania bila ajali inawezekana , timiza wajibu wako’ yatafanyika katika Uwanja was CCM Kirumba jijini humo.

Malima Kabondo, akiwa na wasanii wake kutoka Maringo Bendi wakitumbuiza katika shughuli ya kitaifa iv karibuni.

Akizungumza na Mtanzania Digital , jana kwa njia ya simu, Malima amesma katika maadhimisho hayo pia ataambana na wasanii wake wanaotoka kwenye bendi yake inayoitwa ‘Maringo Band’ ili kusherehesha zaidi siku hiyo.

Nashukuru viongozi wangu wa kazi kuniteua kutumbuiza katika siku hii muhimu ya kuwakumbusha watanzania kuhusu usalama wao pindi wakiwa barabarani iwe kwenye vyombo vya usafiri au watembea kwa miguu.

“Wimbo wa Usalama barabarani Ni miongoni mwa nyimbo nane zilizopo katika albamu ya usalama barabarani niliyo itoa mwaka hun, ambapo lengo ni kuhimiza umakini kwa watu wote wanaotumia barabara katika mizunguko yao ya kila siku.

“Nyimbo nyingine katika albamu hiyo ni biashara na uwekezaji, migogoro, kwanini tunauana, shule ni kusoma, ukatili na ubakaji, fumanizi la nini pamoja na wimbo wa soma uelimike, ambao dhima yake kuu ni kuwakumbusha watu kuendelea kuwekeza zaidi kwenye elimu waelimike,” alisema Malima.

Malima ambaye pia ni Staff Sergeant wa Polisi, Makao Makuu ya Polisi Dodoma, ni miongoni mwa wasanii wakongwe nchini aliyejipatia tuzo tano za Kili awards kupitia wimbo wake pendwa wa ‘ndolela chaseleleka’ uliotamba nchini katika miaka ya 2000 na kumpa umaarufu mkubwa mpaka Sasa.

“Tuzo ya sita niliipata nchini India mwaka 2018 katika Jimbo la Kerela, kwahiyo nashukuru sana viongozi wangu katika Jeshi la Polisi kwa kutambua mchango wangu katika kuelimisha jamii kupitia sanaa yangu.

“Tangu nianze sanaa adi mda huu sikuwahi kukata tamaa licha ya kuwepo changamoto ndogondogo ambazo huwa nazikabili , pia nashukuru kupitia sanaa yangu kuna mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutambulika na viongozi wakubwa kitaifa, pia huwa napata mialiko ya kutumbuiza katika shughuli mbalimbali za kitaifa na watu binafsi kama sherehe za harusi na nyinginezo,” alisema Malima Kabondo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles