24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Malecela atamba CCM kusuluhisha Sudan Kusini

MALECELA.NA PENDO MANGALA, DODOMA
MWANASIASA mkongwe na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Malecela, amesema kitendo cha chama hicho kuwa mwenyeji katika mkutano wa usuluhishi wa mgogoro wa Sudan Kusini, anaamini ni moja ya mambo yatakayokisogeza mbele.
Malecela aliyekuwa msuluhishi wa mgogoro huo, alitoa kauli hiyo jana mjini hapa, wakati akiwashukuru wanaCCM wa Mkoa wa Dodoma kwa mapokezi makubwa, kwani ni heshima kwake na taifa.
“Kiukweli kazi ile ilikuwa ni ngumu sana kwani kusuluhisha watu wanaogombea utawala sio jambo dogo ndugu zangu, namshukuru sana Rais Jakaya Kikwete kwa kuona umuhimu wangu kuniteua mimi kwenda Sudan kusuluhisha mgogoro ule wa wana Sudan Kusini.
“Ikumbukwe mgogoro wa nchi ile ya Sudan Kusini ulianza miaka 1,000 iliyopita na ugomvi mkubwa upo katika suala la kugombania madaraka, hivyo ilikuwa kazi ngumu kuwasuluhisha watu wakiwa wamebeba silaha,” alisema.
Kwa upande wao, wanaCCM wa Mkoa wa Dodoma walimpongeza Malecela kwa kazi hiyo na kudai kuwa ni hazina ya kutegemewa kwa chama na taifa.
Mmoja wa wanachama hao, Anthony Kanyama, ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), alisema mwanasiasa huyo mkongwe ametoka katika kazi ngumu ya kuunganisha watu ambao wanagombania utawala, ni kazi ya hatari, hivyo anastahili pongezi.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles