21.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

MALAYSIA: WAZIRI MKUU WA ZAMANI ASHITAKIWA

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Malaysia Najib Razak amekanusha mashitaka yote dhidi yake wakati alipofikishwa leo mahakamani kuhusiana na kesi ya ulaghai ya mabilioni ya dola.

Razak (65) alikabiliwa na moja kati ya kesi kadhaa kuhusiana na wizi wa fedha za hazina ya kitaifa, inayofahamika kama 1MDB ambao ni mpango wa taifa wa uwekezaji ulioanzishwa kwa ajli ya kuboresha uchumi wa taifa hilo la Kusini mashariki mwa Asia.

Waziri huyo mkuu wa zamani na washirika wake wanatuhumiwa kwa ubadhirifu wa mabilioni ya dola kutoka kwenye hazina hiyo na kuzitumia katika ununuzi wa majumba ya kihafari, kazi za sanaa ya uchoraji na boti za kifahari.

Alitarajiwa na wengi kushinda kwa urahisi muhula mwingine mwaka jana na kuendeleza uongozi wa miongo sita wa muungano wake madarakani, lakini akaangushwa na bosi wake wa zamani, Mahathir Mohamad, ambaye alishinda kwa kutumia hasira ya umma kuhusiana na kesi hiyo ya ufisadi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,717FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles