29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

MALAIKA APATA DILI KUBWA ULAYA

 

 

Na Badi Mchomolo,

Msanii wa muziki nchini Tanzania, Diana Exavery (Malaika), amefanikiwa kupata mkataba na kampuni ya Arban Europe, itakayokuwa na jukumu la kusimamia kazi zake za muziki.

Licha ya kusaini mkataba huo kwa miaka mitatu, pia anatarajiwa kuhamia Ulaya kwa ajili ya kuendeleza kazi zake za kimuziki.

Akizungumza na Mtanzania jana, alipotembelea ofisi za gazeti hili zilizopo Sinza Kijiweni, Jijini Dar es Salaam, Diana alisema licha ya mkataba huo, pia atakuwa akiandikiwa kazi zake za kimuziki na mmoja wa waandishi wa mwanamuziki, Celine Dion.

“Ninashukuru nimefanikiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Arban Europe, ambayo itaweza kusimamia kazi zangu, kampuni hiyo ilikuja nchini kutafuta wasanii wasio na majina makubwa na wasio na uongozi nikapatikana mimi,

“Mazungumzo yangu na kampuni hiyo yamekuwa mazuri na wamedai kuwa watanikutanisha na watunzi wakubwa ambao waliweza kufanya kazi na baadhi ya wasanii nchini Marekani, akiwemo Celine Dion na wengine wengi, nadhani nitakuwa nikipiga hatua kubwa kimataifa,” alisema Malaika.

Malaika aliongeza kwamba licha ya kuwa Ulaya, pia atakuwa akiandaa nyimbo zake zitakapokuwa zikichezwa nchini.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,682FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles