25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Makundi yanayopigania demokrasia yashinda uchaguzi Hong Kong

CENTRAL, HONG KONG

UCHAGUZI wa Mabaraza ya Wilaya kwenye mji wa Hong Kong umekamilika huku kiongozi wake, Carrie Lam akikiri kuwa ushindi wa kishindo kwa makundi yanayopigania demokrasia umeonesha jinsi raia wasivyoridhishwa na utawala wa mji huo.

Makundi hayo yanayopigania demokrasia yamejipatia ushindi wa kishindo baada ya eneo hilo kukumbwa na maandamano ya karibu miezi sita baada ya serikali kupeleka bungeni muswada unaotaka raia wa Hong Kong kushitakiwa China.

Pamoja na kwamba muswada huo ulikuja kuondolewa baadae lakini waandamanaji walikuwa wameanzisha hoja nyingine za kudai demokrasia.

Idadi ya waliopiga kura katika uchaguzi huo walikuwa ni zaidi ya milioni 2.94 ikiwa ni kubwa zaidi ukilinganisha na ile ya mwaka 2016 ambapo walikuwa ni karibu milioni 1.47.

Makundi yanayopigania demokrasia yameshinda viti 390 kati  452 vya mabaraza.

Akizungumzia matokeo hayo jana, Lam alisema kwamba uchaguzi huo umeakisi manung’uniko ya umma juu ya hali iliyopo sasa mjini Hong Kong pamoja na matatizo ya msingi ndani ya jamii.

Amesema Serikali yake itaheshimu na kufanyia kazi sauti ya watu wa Hong Kong katika uchaguzi uliofanyika juzi, ambao umeshuhudia vyama vinavyounga mkono demokrasia vikishinda wingi wa viti kwenye mabaraza yote 18 ya wilaya.

Ingawa mabaraza ya wilaya yana wajibu zaidi wa kushughulikia masuala ya jamii, huwakilishwa pia katika kundi la wajumbe 1,200 ambao watamchagua kiongozi mpya wa Hong Kong mwaka 2022.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles