30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 9, 2022

Makonda azuia Kampuni ya Nyanza kutopewa zabuni

Brighiter Masaki -Dar es salaam

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amepiga marufuku Kampuni ua ukandarasi ya Nyanza aliyepewa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kivule na Kitunda kutopewa zabuni ya kazi ya ujenzi ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Agizo hilo alilitoa juzi  alipotembelea eneo hilo ili kuangalia shughuli za ujenzi zinavyoendelea, ambapo ameonesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa mkandarasi huyo na kuwataka Mamlaka ya Hifadhi za Barabara nchini (TANROADS), mkoani humo kutoipa tena tenda kampuni hiyo.

Akizungumza na waandishi habari pamoja na wakazi wa eneo la Kitunda, Makonda, alisema hataki  Kampuni ya Nyaza ipewe kazi kwani  utendaji wake wa kazi hauridhishi.

“Amebaki kupiga stori tu eti utaalamu utaalamu, ni upumbavu, TANROADS marufuku kuwapa kazi hawa, pesa ya kuwalipa mnayo lakini wanasema utaalamu na mashimo yote haya halafu mnakuja na vitrekta viwili.

“Watu hawana vifaa wameshafanya utapeli na Mradi ukawashinda katika Wilaya ya Temeke mnawapa tena mradi wa Kivule kitunda na nimefatilia ameshawai kufanya kazi na kufanya vibaya mkoani Kigoma na alifanya kwa kusuasua hivyo hivyo sitaki kabisa labda mkuu wa mkoa nisiwe Makonda,” alisema Makonda.

Hivi karibuni mkandarasi huyo alisekwa rumande kwa amri ya mkuu huyo wa mkoa na baada ya siku moja alitolewa kwa dhamana ili aendelee na ujenzi huo, ambapo hadi sasa tayari amekwishalipwa kiasi cha Sh milioni 800.

“Natoa rai kwa mkandarasi wa Barabara ya Kawe namtaka atoe mabipa yale na aweze kufanya kazi yake kwa wakati mana ile barabara tangu naenda kwenye msiba wa mtoto wa kaka yangu Mabeyo (Venance) hadi leo hakuna kinachofanyika nataka kazi.

“Wakandarasi mnaotoa kazi msitoe kazi kwa rushwa ili muweze kufatilia kazi za miradi inayoendelea ukitoa kazi kwa rushwa hautaweza kufatilia kazi zinazoendelea,” alidai Makonda. 

Katika hatua nyingine Makonda ameridhishwa na utekelezwaji wa mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa ya Vingunguti, ambayo yanagharimu kiasi cha Sh bilioni 12.49 na utarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Pia alitembelea mradi wa Soko la Tandale na kumpongeza mkandarasi kwa kufanya vizuri kwani wanakazi mara mbili ya kujenga soko na kuhamisha soko wanaendelea vizuri na utendaji wao wa kazi unaridhisha.

Wakati huo huo Makonda aliwataka wakandarasi wa Kampuni ya Chicco wanaojenga Mto Sinza kwa kuwa wameanza kazi hivyo wafanye kazi kwa bidii usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakadi. 

“Niseme tu kwa sasa hivi mkandarasi hatakiwi kulipwa pesa hadi tutakapoona kazi zake anazozifanya kwa kuwa wengi wao wanataka fedha hakuna wanachokifanya,”  alisema Makonda

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,291FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles