27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Makonda awataka waumini waendelee kuombea amani nchini

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka waumini wa dini ya kiisalmu wakiongozwa na viongozi wao waendelee kuombea amani nchini ili miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa na Rais Dk. John Magufuli itekelezeke kama ilivyopangwa.

Akizungumza leo Jumatatu Desemba 17, jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Makonda amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kuhakikisha amani inaendelea kuweponchini.

Amesema bila kujali tofauti za dini zao kila mmoja kwa imani yake anapaswa aombee amani na kukwepa kutumia dini kuchochea uvunjifu wa amani.

“Wote ni mashahidi wa maendeleo yanayotokea kila kukicha katika jiji letu la Dar esSalam ikiwamo ujenzi na uboreshwaji wa barabara, kujengwa kwa daraja la juu(fly over) yote haya yametekelezwa na Rais Magufuli kwa sababu ya amani,“amesema.

Aidha Makonda amempongeza Rais Magufuli kwa kuendelea kufanya kazi kwa karibu na viongozi wa dini zote nchini bila kujali itikadi zao na hata kujenga msikiti mkubwa kuliko yote Afrika Mashariki unaoatarajiwa kujengwa jijini hapa.

Naye Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema uwepo wa dini mbalimbali nchini ni muhimu kwani ni Taasisi muhimu zinazosaidia kuunga mkono jitihada za serikali katika sekta mbalimbali zikiwamo Elimu na Afya ili kuhakikisha nchi inasonga mbele.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,549FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles