28.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Makonda awapa pole waathirika wa mafuriko

Na BRIGHITER MASAKI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo amefanya ziara ya ukaguzi wa athari za mafuriko ambapo amesema serikali imeanza kukarabati miundombinu iliyoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha ikiwemo madaraja, barabara, mito na mifereji.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo Makonda,  amesema miongoni mwa maeneo yanayoboreshwa na pesa ipo tayari ni mto msimbazi wenye urefu wa km 19 na eneo la Jangwani ambalo maboresho yake yatagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 200 ikiwa ni mkopo kutoka Benki ya Dunia.

Aidha Makonda amesema hadi sasa jumla ya watu wawili wamefariki kutokana na mvua ambapo amewapa pole wananchi waliokumbwa na athari za mafuriko ikiwemo wale ambao mali zao zimeharibiwa na wengine kulazimika kuyahama makazi yao.

“Wananchi mnanaoishi maeneo hatarishi mnanatakiwa kuhama na wakazi wa jiji la Dar es salaam mnatakiwa kufanya usafi katika mazingira yenu ili kuepuka magonjwa ya mlipuko kama Dengue na Kipindupindu “alisema Makonda.

Katika hatua nyingie Makonda amewataka wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Dengue kwa kuhakikisha wanatokomeza mazalia ya mbu na kuhakikisha wanawahi vituo vya afya pindi wanapoona dalili za homa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles