24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Makonda awaasa vijana kutoridhika na mafanikio kidogo

MWANDISHI WETU

KADIRI siku zinavyozidi kwenda, biashara ya mtandao inazidi kukua kwa kasi nchini. Haya ni matokeo ya ongezeko la idadi ya watu na vijana wenye kujituma. Hata hivyo, kuna dhana potofu inayosambaa kwamba biashara hii si halali, huku wengine wakisema ni utapeli.

Watu wengi hawafahamu kuwa hii ni sekta yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 190 ikiwa na zaidi ya wasambazaji milioni 96 duniani kote.

Kampuni ya mauzo ya moja kwa moja ya QNET ni sehemu ya sekta hii, iliyodhibitiwa na sheria, maadili na taratibu za kiutendaji.

Meneja Mkuu wa QNET Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika, Biram Fall, hivi majuzi alitembelea jijini Dar es Salaam na kusema kampuni yao inaendesha biashara halali katika nchi nyingi duniani na kwamba wanatoa bidhaa halisi.

Fall alifika hapa nchini wakati QNET ikifanya maonesho ya Expo, kwa lengo la kutambulisha bidhaa na huduma zao kwa wateja.

Anasema wamekuwa wakiendesha biashara hii kwa zaidi ya miongo miwili hivyo kama isingekuwa halali basi wasingedumu kwa muda huo.

“Mifumo ya Piramidi huwa haidumu kwa muda mrefu kama ilivyodumu kampuni hii, ambayo ilianza kazi mwaka 1998, muda ambao matapeli hawawezi kustahimili,” anasema Fall.

Anabainisha kuwa kampuni hii ina nembo yenye sifa nzuri na inayojulikana duniani hivyo, haiwezi kujihusisha na utapeli wa aina yoyote.

“Watu wabaya wapo siku zote, hii ni changamoto. Lakini kwa suala la kanuni tunawahakikishia biashara katika QNET inaendeshwa kimaadili na kwa sababu hatuko hapa kuwadanganya watu ninawahakikishia itaendelea kuwapo,” anasema Fall.

Anasema QNET ipo kwa ajili ya kuwawezesha watu, hasa vijana.

Kwa mujibu wa Tathmini ya Idadi ya Vijana Afrika iliyofanywa na Taasisi ya Maendeleo ya Afrika (African Institute for Development), Afrika ina zaidi ya asilimia 45 kati ya watu milioni 150 waliopo Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda.

Vijana wengi wana elimu, ufahamu wa teknolojia, uwezo unaoendana na mifumo mipya kwa haraka, juhudi na fikra za ujasiriamali – sifa ambazo ni za msingi zinazohitajika kwaajili ya mafanikio endelevu katika biashara ya mauzo ya moja kwa moja.

Biashara ya masoko ya mtandao au Mauzo ya moja kwa moja ni dhana ya biashara ya kimataifa na inaelezwa kuwa ni uuzaji wa bidhaa au huduma kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, mbali na maduka halisi ya kawaida.

Mtindo huu wa mauzo una upo kwa zaidi ya miaka 100 sasa na ulianzishwa Amerika.

Fall anasema hadi sasa kuna takribani watu milioni 117 wanaohusika katika biashara hii.

Kwa mujibu wa  taarifa ya mwaka ya Shirikisho la Vyama vya  Mauzo ya Moja kwa Moja Duniani (World Federation of Direct Selling Association (WFDSA) ya mwaka jana, biashara ya mauzo ya moja kwa moja ilizalisha Dola za Marekani bilioni 190 na takribani nusu ya mauzo yote yametokea katika masoko yanayochipukia.

Anasema Afrika imechangia chini ya asilimia moja ya jumla ya mauzo ya WFDSA lakini wataalamu wanatabiri kwamba soko la Afrika Mashariki linatoa fursa ya kukua kwa wajasiriamali wenye ari na hata kwa wale wenye kazi za kudumu na wana nia ya kujipatia kipato cha ziada kupitia mauzo ya moja kwa moja.

Katika kanda ambayo matakwa ya ajira rasmi yanazidi kuwa na ushindani na kazi za kudumu kuendelea kuwa kidogo, biashara ya mauzo ya moja kwa moja inatoa njia mbadala ya ajira za kawaida kwa wanaohitaji kipato cha ziada.

Wakati ambapo mtindo huu wa biashara inakabiliwa na changamoto, kubwa zaidi ni kuenea kwa mifumo isiyo halali ya piramidi inayojiwasilisha kama kampuni halali ya biashara ya mauzo ya moja kwa moja.

Hoja ni kwamba; ‘matapeli’ hawa wanajenga dhana potofu kwenye sekta ya mauzo ya moja kwa moja, jambo ambalo linaleta vikwazo kwa kampuni halali kusajili mawakala wa mauzo na kuendesha biashara zao halisi na halali.

Matokeo yake, kampuni inatatua tatizo hilo kwa kuuelimisha umma kuwa makini nao na kuwahamasisha kuthibitisha uhalali wa kampuni yoyote kulingana na inavyotekeleza na kutii kanuni, sheria na taratibu zilizowekwa na bodi zinazosimamia.

Katika kuimarisha uwapo wake nchini, QNET ilifanya maonesho ya bidhaa hapa jijini ambapo pia alikuwapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Akiwa katika maonesho hayo, aliwapa changamoto vijana wanaotafuta fursa kupitia kampuni hii kuwa na ujasiri wanapofanyia kazi ndoto zao ili wapate mafanikio.

Makonda anasema historia ya maisha yake ni ushahidi tosha kwamba kufanya kazi kwa bidii na ujasiri huleta mafanikio hivyo, anaawasa vijana kutotosheka na mafanikio madogo.

Anasema: “Usiridhike kwa mafanikio au vitu vidogo vidogo, hakikisha unatimiza  ndoto zako.”

Maonesho ya bidhaa ya Expo yaliyobeba jina la Kuishi Kikamilifu ‘Absolute Living’ inayoendana na falsafa ya msingi ya kampuni, hufanyika kila mwaka katika nchi tofauti duniani.

“Kutoka katika kozi za elimu kwa njia ya mtandao, (online course) hadi katika kozi za vifurushi vya sikukuu, bidhaa za kuongeza nguvu, vyakula vya nyongeza na saa, tuna aina mbalimbali zinazoweza kutuwezesha kutoa huduma kwa mahitaji ya kila aina.

Katika msingi wa yote haya, ni hamu yetu kutoa  fursa ya ‘kuishi kikamilifu,” anasema Fall.

Kampuni pia inatoa fursa za biashara kwa gharama nafuu kwa watu wanaotaka kuifanya, bila kujali kiwango chao cha elimu.

QNET inaamini kwamba hakuna kinachompa nguvu zaidi mtu kama uhuru wa kifedha unaotokana na kufanya kazi katika sekta ya mauzo ya moja kwa moja na inaweza kuwa kazi ya kujitosheleza kwa wale watakaoamua kuifanya.

Tofauti na biashara zingine za kawaida ambazo zinahitaji mtaji mkubwa wa kuanzisha, rasilimali na hata uzoefu, hii haigharimu fedha nyingi wala haiangalii kiwango cha elimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles