27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Makonda aunda kamati kuikabili Biashara ya ngono, ushoga

   Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameunda kamati ya watu 17 itakayopambana na biashara za ngono, madangulo na ushoga katika mkoa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Oktoba 31 jijini Dar es Salaam, Makonda amesema kamati hiyo itajumuisha wataalamu kutoka mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Jeshi la Polisi.

Wengine watakaounda kamati hiyo ni kutoka Bodi ya filamu, madaktari na wataalamu wa saikolojia.

“Kamati hiyo itashughulikia watu wanaofanya vitendo vya ushoga na wanaotengeneza filamu za ngono ambapo hadi sasa tayari kuna nyumba 24 zinazodaiwa kufanya hivyo, wapo wengine wanafanya biashara za ngono katika mitandao ya kijamii,” amesema Makonda.

Makonda ameongeza kwamba makao makuu ya kamati hiyo ni Mburahati na inatarajiwa kuanza kazi rasmi Jumatatu Novemba 5, mwaka huu.

” Kamati hii itakwenda kushughulikia na watu walioamua kujitangaza na kufanya biashara kupitia mitandao kama James Delicious, Anti Milk, Dida Mtamu, Bariki, Abbas na kundi la Whatsap la Pachupachu,” amesema Makonda.

Ameongeza kuwa pia kamati hiyo itawashughukia wale wanaotapeli kwa njia za mitandao na kwa kutumia majina ya viongozi.

“Niwaombe kuwa mapambano haya si ya serikali ni ya Watanzania wote tushikamane kwa kuwa maadili ya mwafrika si haya ndio maana tukiomba hayafanikiwi ni kutokana na mambo ambayo hayakubaliki katika imani zote,” amesema Makonda.

Amewaomba watetezi wa haki za binadamu kuacha kutetea tabia hizo kwa kuwa kwa sheria za Tanzania nikinyume cha sheria.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles