25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Makonda ataka gereji bubu kurasimishwa

Anna Potinus

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametaka gereji nchini kurasimishwa na kuwa sekta rasmi huku akihimiza mafundi waliokaa muda mrefu gereji kupatiwa vyeti kutokana na kuwa na ujuzi wa kutosha.

Makonda ametoakauli hiyo leo Desemba 5, alipokuwa akizungumza na wamiliki wa gereji jijini Dar es salaam.

“Ndugu zangu turasimishe gereji zetu na nikisema hivyo ninamaanisha kuwa tulipe kodi, wenzenu wamachinga wana vitambulisho ambavyo vinawafanya watambulike na serikali, jambo hili litawafanya mjulikane na wateja pia wataweza kutambua gereji kwa ukubwa hata kama ni ya mtaani.

“Ninataka mafundi wapate vyeti wakiwa wako gereji mbali na wale wanaotoka vyuoni kwasababu unakuta mtu yupo darasani miezi mitatu anapata cheti ila yule aliyekaa gereji muda mrefu hana cheti halafu ana ujuzi wa kutosha tofauti na yule wa darasani.

“Tunaposema kurasimisha haimaanishi kwamba utoke ulipo na uhamie sehemu nyingine hapana ila tunataka serikali ikutambue ulipo pia tunawaomba sana mtoe risiti kwa wateja wenu baada wa kuwapa huduma ili tuweze kuondokana na zile gereji bubu zote.

Aidha amewataka wamiliki na mafundi wa gereji kuwa na jicho la usalama akidai kuna watu wanaoenda katika gereji zao kubadilisha vipuli baada ya kuiba au vifaa vinavyoibiwa kwenda kwao na hivyo kuwataka wawe walinzi na watoe taarifa kwa vyombo vya usalama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles