25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Makonda aongoza mazishi ya Kivamwo

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda.

MAULI MUYENJWA NA LEONARD MANG’OHA, DAR ES SALAAM

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda jana ameongoza na viongozi mbalimbali  kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari, Adolf Kivamwo ambaye mazishi yake yalifanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa  kuaga mwili wa marehemu Kivamwo, Makonda alisema ni vizuri kumkumbuka kwa mema aliyoyafanya ikiwa ni pamoja na kuendeleza mambo mazuri aliyoyaacha.

“Hii ni safari ya wote, marehemu aliishi na sisi vizuri tumuombee Mungu, ni vizuri kumuenzi kwa mambo mema ambayo alikuwa akiyafanya katika jamii,”alisema.

Kutokana na kuguswa na msiba huo, Makonda aliahidi kuwalipia ada watoto wa marehemu Sh milioni 4 mwaka huu.

Viongozi wengine, waliokuwapo ni Mbunge wa Chalinze,Ridhiwani Kikwete (CCM), Mbunge wa Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji,Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea (Chadema), Mwenyekiti wa Makampuni ya  IPP na  Dk.Regnald Mengi.

Marehemu  Kivamwo alifariki dunia Septemba 23, mwaka huu kwa maradhi ya saratani aliyokuwa akiuugua muda mrefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,436FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles