22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Makonda aja na mpango kumbukumbu za ndoa Dar

BRIGHITER MASAKI-DAR ES SALAAM

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ametangaza mpango madhubuti ikiwamo kuanzisha mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu zote za ndoa.

Amesema ndoa zote zilizopo katika mkoa wake kumbukumbuku zake zitahifadhiwa ili kupunguza utapeli wanaofanyiwa wanawake kwa kudanganywa na wanaume kuwa wataolewa matokeo yake kuwaacha na maumivu.

Akizungumza na waandishi wa habari, jana Makonda alisema kuwa, mbali ya mipango hiyo, atatumia mkutano wa SADC  unaoendelea nchini kupata uzoefu kutoka kwa nchi nyingine kufahamu namna gani wanakabiliana na utapeli wa aina hiyo.

“Nimesikia na kupata malalamiko kwa wanawake wengi wamekuwa wakitapeliwa na kudanganywa na wanaume kuwa wataolewa na kutelekezwa sasa kutakuwa na kanzidata itakayosaidia kumtambua mtu kama ameoa au bado,” alisema

Alisema kituo hicho cha kuhifadhi kumbukumbu  kitahusisha usajili wa ndoa zote ili wanaume waliooa waweze kutambulika na kuwanusuru ili wasitapeliwe na kuumizwa mioyo yao kwa mifadhahiko ya kutegemea ndoa hewa.

“Kanzidata hii itawasaidia wanawake wasitapeliwe, mtu akitaka kukuoa utaenda mtandaoni na kuangalia taarifa zake, utabaini kama ameoa au la na vilevile itawasaidia hata wanawake ambao wameolewa ili kuzuia waume zao wasioe kwa siri, na kuwadanganya wengine,” alisema MakondaMARAIS SADC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles