29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Makonda aipigia debe TTCL

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amezitaka taasisi na mashirika ya umma mkoani hapa  kuiunga mkono Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kutumia mawasiliano yanayotolewa na kampuni hiyo.

Makonda alitoa kauli hiyo    Dar es Salaam  jana alipokuwa akizindua wiki ya huduma kwa wateja wa TTCL.

“Serikali imeonyesha nia njema ya kuirejesha TTCL katika hali nzuri baada ya kuimiliki kwa asilimia 100.

“Kwa hiyo  litakuwa jambo la busara na la heshima kama mashirika na taasisi za umma zilizoko Dar es Salaam  zitaunga mkono juhudi za Rais, Dk. John Magufuli za kuirejesha kampuni hiyo chini ya umiliki wa Serikali kwa asilimia 100.

“Katika hili, mimi kama kiongozi wa mkoa nitahakikisha ofisi zote za umma zilizopo chini yangu zinatumia huduma za TTCL  kuimarisha uzalendo.

“Kama kuna ofisi yoyote ya umma itasita kutekeleza jambo hili, naomba mniambie   niingilie kati kwa sababu hakuna sababu ya kutojali bidhaa zetu wenyewe,” alisema Makonda.

Makonda pia alizitaka taasisi za umma zinazodaiwa na kampuni hiyo zilipe madeni yao  kampuni hiyo iweze kujiendesha kwa mafanikio.

“Kama wadaiwa watashindwa kulipa madeni yao  basi wafikisheni mahakamani  wakalipie huko,” aliagiza Makonda.

 

Naye Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba, alisema TTCL ilianza mchakato wa kuleta mabadiliko tangu mwaka 2014 kwa mpango uliopewa jina la TTCL Business Transformation Project.

 

Kwa mujibu wa Kindamba, mpango huo ulilenga kuongeza utendaji na ufanisi katika uzalishaji na uwajibikaji   kutoa huduma bora kwa wateja wa kampuni hiyo.

 

Kuhusu Wiki ya Huduma kwa Wateja, alisema inalenga kutambua na kuthamini mchango wa wateja ambao wamekuwa chachu ya kukua kampuni hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles