25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MAKONDA AELEZA DAWA ZA KULEVYA ZINAVYOINGIA

Na mwandishi wetu – Dar es Salaam

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameeleza namna dawa za kulevya zinavyoingia na kutoka nchini, wakati akitaja orodha ya watu 65 aliowataka kuripoti polisi wakihusishwa na dawa hizo.

Makonda alisema njia rahisi inayotumiwa kuingiza na kutoa dawa za kulevya nchini ni Dar es Salaam, Zanzibar, Bagamoyo mkoani Pwani na Tanga.

Alisema wafanyabiashara wamekuwa wakitumia mbinu tofauti tofauti kama kuzisafirisha kwenye meli za mafuta, meli zinazobeba magari ama kuwatumia watoto wa kike kuzibeba kwa ujira wa Dola za Marekani 7,000.

“Wakati mwingine dawa zinawekwa kwenye mifuko ya sukari alafu zinaingizwa kwenye mapipa, zinapakiwa kwenye meli, zikifika maeneo ya karibu na huku, yale mapipa yanatoswa habarini huku yakiwa yamefungwa GPRS (kifaa maalumu cha mawasiliano), meli zikifika huku zinakuwa hazina kitu, wale watu wanawasiliana na wenye mizigo yao, wanaondoka mpaka yalipo yale mapipa kwa sababu yana GPRS inawaonyesha, wakifika wanazama na kuyachukua.

 “Zikishatolewa hapo zinapelekwa Mtwara, kisha zinasafirishwa tena hadi Afrika Kusini. Wengine wananunua magari Japan wanayapeleka Bombay India au Karachi Pakistan, wanafungua baadhi ya maeneo ndani wanaficha zile dawa kisha magari yanakuja.

“Wengine wananunua magari Japan wanayapeleka Amerika ya Kusini wanafunga baadhi ya maeneo kwenye gari wanazifungia ndani kisha wanayaleta, kwa hiyo ukiangalia unaona gari limepita sehemu kubwa mpaka kufika, kwa hiyo ukisikia sehemu fulani wanauza magari bei rahisi kumbe kuna biashara nyingine,” alisema.

Makonda aliendela kusema: “Kuna dada mmoja ana maduka Sinza na Tanga, huwa anawatumia wasichana kwa kuwabebesha dawa za kulevya kwa ajili ya kupeleka China, anawapa Dola za Marekani 5,000 na ukifanikiwa kuingiza mzigo unalipwa Dola za Marekani 7,000. Tayari kuna wasichana wawili wamefungwa China,” alisema Makonda.

Alitaja mbinu nyingine inayotumiwa na wafanyabiashara hao kuwa ni kukipasua kitunguu maji katikati kisha kuweka dawa za kulevya na kukifunga tena kwa gundi.

“Unakuta mtu anasafiri kutoka China anafika Uwanja wa Ndege anakutana na mtu anamuomba amuuzie kilo zake za mzigo kwa gharama ya Dola za Marekani 100 hadi 200 halafu unaandikwa kwa jina lako, ukifika Dar wana mtu wao maalumu wa kuja kupokea na akichelewa kuja kuuchukua unashangaa umekamatwa, hivyo watu wachukue tahadhari,” alisema.

Pia alisema maeneo kati ya Kimara na Mbezi Mwisho yamekuwa yakitumika kushusha mizigo aliyodai kuwa ni ya dawa za kulevya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles