30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 9, 2022

Makonda aagiza maduka kufunguliwa saa tano leo

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza maduka yote kufunguliwa kuanzia saa tano asubuhi leo ili kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa vitendo kwa kujiandikisha kwa wingi katika daftari la mpiga kura kwa lengo la kupata haki ya kuwapigia kura viongozi wa Serikali za Mitaa.

Taarifa iliyotolewa jana ilieleza kuwa hatua hiyo kama njia ya kumuenzi Mwalimu Nyerere pia ni sehemu ya kuwahamasisha wananchi kujiandikisha kwenye uchaguzi.

“Kesho Oktoba 14 (leo) ni kumbukizi ya miaka 20 tangu Baba wa Taifa atangulie mbele za haki,na kwakuwa kesho ni siku ya mwisho ya kujiandikisha katika daftari la mpiga kura kuwapata Viongozi wa Serikali za Mitaa, kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kukuza demokrasia ndani ya mkoa wetu na nchi yetu kwa ujumla.

“Naelekeza maduka yote yafunguliwe kuanzia saa tabo asubuhi hapa Dar es Salaam kwa kuwa hii ni sehemu ya kumuenzi Baba wa Taifa katika kuhakikisha wote tunajiandikisha ili kupata haki ya kupiga kura maana Baba wa Taifa aliwapa nafasi kubwa viongozi hawa wa Serikali za Mitaa.

“Baba wa Taifa alithamini viongozi wa mitaa kwa kuwa ni nguzo kuu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali, tumuenzi kwa kujiandikisha, wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Dar es Salaam, maduka yatafunguliwa kuanzia saa tano asubuhi na unapofungua duka hakikisha wewe mwenyewe umejiandikisha, niwaombe wamachinga, bodaboda, viongozi wa taasisi za Serikali na binafsi, wanafunzi waliotimiza miaka 18 ni fursa pekee tutumie leo na kesho tujae kwa wingi vituoni,” alisema

Makonda amewataka pia wamiliki wa baa na sehemu nyingine za starehe kuwahamasisha wanaofika kwenye maeneo yao kujiandikidha kwakuwa kupiga kura ni haki ya msingi ya kila raia wa Tanzania.

“Ndugu zangu wenye klabu, bar na sehemu zote za Starehe naomba wahamasisheni watu wenu kwenye maeneo yenu kuhakikisha wamejiandikisha na kesho miongoni kwa maeneo nitakayoyatembelea ni pamoja na baa ni matumaini yangu nikifika baa nitakukuta ukiwa tayari umejiandikisha,” alisema Makonda

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,291FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles