30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MAKOMANDOO KUPAMBA SHEREHE ZA MUUNGANO

Na Lilian Lundo- MAELEZO


MAONYESHO ya ukakamavu na mbinu za medani katika kupambana na adui, hasa kulinda amani ya nchi yetu kutoka Kikosi Maalumu cha Makomandoo wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), itakuwa ni sehemu ya shamrashamra zitakazopamba maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yatakayofanyika kwa mara ya kwanza mjini Dodoma, Aprili 26.

Taarifa iliyotolewa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, ilieleza kuwa maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na Rais Dk. John Magufuli.

Waziri Mhagama alitaja shughuli nyingine zinazotarajiwa kufanyika siku ya Muungano kuwa ni gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama (JWTZ, JKT, Polisi na Magereza) na onyesho la mbwa na farasi waliofunzwa.

 “Kauli mbiu ya sherehe za kutimiza miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni ‘Miaka 53 ya Muungano; Tuulinde na Kuuimarisha, Tupige Vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii’,” alisema.

Alitoa wito kwa wananchi wote nchini kusherehekea siku hiyo muhimu kwa kudumisha amani, upendo, umoja na mshikamano kwa maendeleo ya nchi.

Maadhimisho ya Muungano yanafanyika kwa mara ya kwanza Dodoma ikiwa ni siku kadhaa tangu Serikali ya Awamu ya Tano ianze kutimiza azma ya kuhamia katika makao makuu hayo mapya. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles