30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Makinda: kasi ya uhamasihaji watu kujiunga CHF hairidhishi

Julieth Peter, Babati

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anna Makinda, amesema haridhishwi na kasi ya uhamasishaji wa watu kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ulioboreshwa (CHF) kwa lengo la kupata matibabu mwaka mzima pindi wanapougua.

Makinda ameyasema hayo wilayani Babati mkoani Manyara wakati akizindua zoezi la siku sita la utoaji wa huduma za matibabu linalofanywa na madaktari bingwa wanane kutoka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Benjamini Mkapa kwa wanachama na wasio wanachama wa NHIF.

“Inashangaza kuona Manyara kitakwimu ndiyo mkoa unaoshika nafasi ya mwisho wa watu kujiungana bima ya afya kwa asilimia saba miongoni mwa mikoa mipya na kwamba ikilinganishwa na Mkoa wa Songwe ulioanzishwa mwaka juzi inashika nafasi ya kwanza kwa kuongoza kwa asilimia 86 kati ya mikoa yote nchini.

“Hiisi nzuri inawezekana hatujui ni mbuzi mmoja unayemuuza kwa Sh 60,000 unatakiwa kutoa Sh 30,000 tu kujiunga na bima ya afya na kupata matibabu familia nzima kwa mwaka mzima,” amesema.

Makinda alibainisha Mpango huo kuwa ni  lengo la Serikali la kuhakikisha kila Mtanzania anajiunga na mojawapo ya bima ya afya  pindi anapougua aweze kupatiwa matibabu kwa urahisi hata pale wanapokuwa hawana fedha.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles